Header Ads Widget

TTCL SINGIDA YAWAITA WANANCHI KUCHANGAMKIA VIFURUSHI VYA BEI NAFUU



Na Thobias Mwanakatwe, SINGIDA


SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limewataka wananchi wa Mkoa wa Singida kuchangamkia huduma mpya za vifurushi kikiwamo kinachojulikana kwa jina la ‘BUFEE PACK’ ili waweze kupata huduma bora na nzuri za mawasiliano.


Meneja wa TTCL Mkoa wa Singida, Augustino Mwakyembe alisema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya WALETE mkoani hapa ambayo ina lengo la kufikisha mawasiliano ya simu za mkononi kwa wakazi wa Singida kwa bei nafuu.


Alisema kifurushi cha Bufee Pack kinampa mteja fursa ya kujichagulia kiwango cha muda wa maongezi, huduma ya data na ujumbe mfupi kulingana na mahitaji yake.


Alisema kwa kumjali mteja wao zaidi, Kifurushi cha BUFEE ambacho kimeanza tangu mwaka jana  hakina ukomo wa muda ambapo mteja atatumia kifurushi chake mpaka kitakapoisha kabisa huku akipewa taarifa kulingana na matumizi. 


Mwakyembe alisema pia kipo kifufushi kinachotwa JIACHIE ambacho nacho mteja anatumia bila kikomo hivyo hakuna sababu yeyote kwa wananchi wa Mkoa wa Singida kupitwa na huduma zinazotolewa na TTCL.



"


Alisema katika kipindi cha miaka miwili wananchi wamehamasika na matumizi ya huduma za TTCL kutokana na ubora wa huduma ambapo kwa Mkoa wa Singida kuna minara takribani 29 ambayo imefanya mawasiliano yawe bora zaidi.


"Huduma za TTCL zimeboreshwa sana kutokana na uwingi wa minara ambapo zamani tulikuwa tunatumia  2G lakini sasa tunatumia 4G katika huduma ya intaneti," alisema.


Mwakyembe aliongeza kuwa TTCL katika kipindi cha mwaka huu imejipanga zaidi kwa kuhakikisha inafikisha huduma zilizobora kwa wananchi wa Mkoa wa Singida.


Aidha, Mwakyembe alitoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Singida kulinda miundombinu TTCL isihujumiwe na wanapoona kuna hujuma watoe taarifa kwa vyombo vinavyohusika ili hatua zichukuliwe kwa wahusika.


"Serikali inatumia fedha nyingi sana kujenga miundombinu ya TTCL kwa hiyo ni jukumu la wananchi kuhakikisha wanailinda isihujumiwe na watu wasiokuwa na nia njema na shirika," alisema.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI