Header Ads Widget

KIGOMA KINARA KUPOKEA PESA ZA MIRADI

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MKOA Kigoma unaelezwa kuwa mkoa unaoongoza nchini kwa kupatiwa fedha nyingi za utekeleza miradi ya maendeleo kwa kipindi cha miaka minne ya Rais Samia Suluhu Hassan madarakani.

Naibu Waziri wa nchi ofisi ya Raisi Tawala za mikoa na serikali za mitaa, Zainab Katimba alisema hayo katika kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa kilichofanyika mjini Kigoma akieleza kuwa fedha hizo zinalenga kutekeleza mpango wa kuufanya mkoa huo kuwa kitovu cha uchumi na biashara.

Katimba alisema kuwa tangu aingie madarakani Raisi Samia ameutizama mkoa Kigoma kipekee na hasa baada ya kuwa nyuma kwa miradi na kimaendeleo na hivyo alisema kuwa viongozi na wananchi wa mkoa Kigoma hawana budi kumuunga mkono Raisi Samia

Akizungumzia kauli hiyo ya Naibu Waziri wa TAMISEMI Mkuu wa mkoa Kigoma, Thobias Andengenye amekiri mkoa huo kupokea kiasi cha shilingi Trilioni 11.5 kwa kipindi cha miaka minne ambacho Raisi Samia yupo madarakani na miradi mikubwa ya kimkakati imeanza kutekelezwa na kwamba miradi yote iliyokusudiwa inaendelea na utekelezaji.

Andengenye alisema kuwa kwa namna Raisi Samia alivyowezesha upatikanaji wa fedha hizo mkutano huo unaunga mkono azimio la Kumshukuru na Kumuunga mkono na kwamba serikali ya mkoa itasimamia kwa karibu kuona fedha hizo zinakwenda kutekeleza miradi ambayo inagusa maisha ya wananchi.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa mkoa Kigoma, Hassan Rugwa alisema kuwa fedha zilizotolewa na Raisi Samia kwa ajili ya utekelezaji miradi zinalenga kuboresha utoaji huduma, kuchochea halmashauri na taasisi za serikali kuongeza ukusanyaji mapato kwa asilimia 25 na kwamba fedha hizo pia zinalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kuongeza mzunguko wa fedha kwenye shughuli zao.

Mwenyekiti wa CCM mkoa Kigoma, Jamal Tamim alisema kuwa kazi kubwa aliyofanya Rais Samia inaonekana kwenye utekelezaji wa miradi hivyo watanzania wote kwa kauli moja wanapaswa kuunga mkono azimio la Mkutano Mkuu wa CCM wa kupitisha Raisi Samia, Dk.Hussein Ally mwinyi na Katibu Mkuu wa CCM, Emanuel Nchini  kuwa wagombe   wa nafasi za Uraisi kupitia chama cha Mapinduzi.










Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI