Header Ads Widget

TEA YAKABIDHI VYOO MATUNDU 24 KWA TSHS. MILIONI 51 MPECHI SEKONDARI NJOMBE

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE 


Zaidi ya shilingi Milioni 51 zilizotolewa na Mamlaka ya Elimu Tanzania TEA zimetekeleza mradi wa ujenzi wa Vyoo matundu 24 katika shule ya Sekondari Mpechi Halmashauri ya mji wa Njombe mkoani Njombe na kupunguza changamoto ya watoto kuugua magonjwa yanayotokana na uchafu.


Akikabidhi mradi huo Mratibu wa miradi Toka TEA Consolatha Mosha amesema Mamlaka hiyo imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali kwenye shule na mradi wa matundu ya Vyoo ulitokana na maombi ya Shule yenyewe.


Mkuu wa shule ya Sekondari Mpechi Mwalimu Brown Kiswaga na wanafunzi wamekiri kunufaika na mradi huo ambao umekuwa mkombozi katika kuondokana na kukosa baadhi ya Vipindi kutokana na kuugua maradhi yanayotokana na uchafu ikiwemo UTI.


Wananchi wa Mtaa wa Mpechi Mjini Njombe na Diwani wa kata ya Mjimwema Nestory Mahenge wameishukuru Mamlaka ya Elimu Tanzania kwa kujenga Vyoo katika shule hiyo kwani awali watoto walikuwa wanataabika kujisitiri Hali iliyokuwa ikichagiza utoro kwa baadhi yao.


Kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini,Andreas Mahali katibu wa Mbunge huyo anasema kinachofanywa na TEA kinaongeza chachu kwa watoto kufanya vizuri katika masomo yao.


Mkoa wa Njombe umepata Zaidi ya shilingi  bilioni 1.19 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali Toka Mamlaka ya elimu Tanzania TEA






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI