Header Ads Widget

TEA YATENGA BILIONI 3 UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU SHULE 20 NCHINI

 



Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima App Dodoma


MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Erasmus Kipesha amesema katika kutekeleza Sera mpya ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 toleo la Mwaka 2023, Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imetenga shilingi bilioni 3 kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu na vifaa mbalimbali vya mafunzo ya amali kwa shule 20 nchini.


Ameyasema hayo leo Februari 25, 2025, katika ofisi Idara ya Habari - MAELEZO, Dodoma wakati akizingumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita 


Dkt,Kipesha amesema kuwa wajibu wao ni kuhakikisha wanaunga mkono utekelezaji wa Sera hiyo ya Elimu kwa kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa maana ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, maabara za Sayansi, nyumba za walimuna vifaa mbalimbali vya mafunzo ya amali kama michezo, ushoni, mapishi, kilimo, sanaa na TEHAMA


Aidha amesema kuwa watahakikisha wanaimarisha miundombinu ya elimu kote nchini kuunga mkono utekelezaji wa sera ya elimu kwa kuwa na miundombinu na vifaa vya mafunzo ya amali.


"Jukumu letu kubwa ni kuimarisha na kuboresha miundombinu ya kujifunzia na kufundishia kwa kujenga vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo, nyumba za walimu, maabara, mabweni pamoja na kuweka vifaa mbalimbali vya elimu vya mafunzo ya amali, " Amesema.



Na kuongeza kuwa "Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuwakomboa vijana wa Kitanzania kwa kuboresha sera ya elimu na mafunzo ambapo vijana wengi wataweza kujiajiri au kuajiriwa mahali popote nchini kulingana na ujuzi watakaoupata mashuleni, " Amesema


Sambamba na hilo Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa wadau mbalimbali nchini kuendelea kuiunga mkono Serikali kwa kuchangia sekta ya elimu kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa.


"Kuna faida ya kuchangia maendeleo ya elimu kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa ila hatuwalazimishi kupitia TEA ila kwa namna yeyote ambavyo mdau atachangia lengo ni kuendeleza sekta ya elimu," ameeleza Dkt. KIPESHA








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI