Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema kuanzia February 18 hadi February 22,2025 limewakamata
Watuhumiwa 26 wakiwemo Najim Issa Houmud Mkurugenzi (34) Mkazi wa Kigamboni, Hatibu Kudura miaka (25) Mkazi wa Kinondoni, Fatum Hamisi (26) Mkazi wa Kigamboni na Athumani Sadik (29) Mkazi wa Mabibo kwa tuhuma za kujihusisha na biashara haramu ya upatu mtandaoni bila kuwa na kibali kutoka Benki Kuu Tanzania.
Taarifa iliyotolewa na Polisi leo February 24,2025 imesema Watuhumiwa hao walikamatwa katika maeneo ya Mbagala, Gongolamboto, Tabata, Mbezi Magufuli, Ubungo Riverside na Mabibo ambapo Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania lilifanya
uchunguzi wa kampuni LEO BURNETT LONDON (LBL) inayo jihusisha na biashara ya upatu
mtandaoni na kubaini kuwa kampuni hiyo haina uongozi maalum, vilevile ufanyaji kazi wake ili uweze kujiunga ni lazima utoe kiasi cha pesa kuanzia Tsh, 54000 na kuendelea ili uwe Mwanachama, pia huchangisha pesa kwa kuwadanganya Wananchi kuwa watapata faida kubwa kwa muda mfupi bila ya Wanachama kuhusishwa kwa namna yoyote katika shughuli za uendeshaji wa kampuni hiyo.
“Mara upelelezi utakapokamilika Watuhumiwa wote watafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma
zinazowakabili, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa Wananchi wote kuacha kujihusisha na biashara za upatu mitandaoni bila kujiridhisha kwanza kwa kuwa baadhi ya biashara hizo hazina leseni wala vibali kutoka Mamlaka za kisheria zinazohusika hivyo kuhatarisha usalama pesa zao”
0 Comments