MKUU wa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma Dinnah Mathamani (kulia) akiongea na Shauri John.
Na Fadhili Abdallah, Kigoma
MKUU wa wilaya Uvinza Dinnah Mathaman amesema kuwa mdau yeyote wa elimu anayetaka kumchukua mtoto Shauri John aliyetrend kwenye mitandao ya kijamii ambaye anataka kumchukua mtoto huyo kutoka kwa wazazi wake ili amsomeshe anapaswa kufuata taratibu za kisheria za kumkuchukua mtoto huyo ikiwemo kupata ridhaa ya wazazi na kibali cha serikali wilayani humo.
Mathamani alisema hayo akitoa maelekezo ya serikali kufuata wadau mbalimbali waliojitokeza kutaka kumchukua mtoto huyo akiwemo Mkuu wa wilaya Kisarawe mkoani Pwani, Petro Magoti baada ya kumuona mtoto huyo akizungumza kwenye mitandao ya kijamii akieleza kiu yake ya kutaka kusoma badala ya kuchunga mifugo ya wazazi wake kama anavyofanya sasa hivi.
Akizungumza katika shule ya Msingi Kahwibili iliyopo kijiji cha Kahwibili kata ya Rukoma wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma Mkuu huyo wa wilaya Uvinza alisema kuwa serikali haimzuii mdau yeyote kumchukua mtoto huyo lakini amesisitiza kuwa lazima ridhaa ya wazazi na kibali cha serikali vifuatwe ili kuzingatia usalama wa mtoto huyo mahali atakapokuwa.
kizungumza shuleni hapo Mwanafunzi huyo Shauri John alisema kuwa alilazimika kwenda kuchunga mifugo ya baba yake baada ya kuona shuleni kwao hakuna walimu muda mwingi walikuwa wanacheza hivyo akawa anaenda kuchunga mifugo ya baba yake.
Hata hivyo mtoto huyo alisema kuwa ana hamu ya kusoma na kutimiza ndoto yake lakini hayuko radhi kwa sasa kusomea kijijini huko kwani hataweza kusoma vizuri na kufaulu kama ndoto zake zilivyo za kutaka kuwa Mhandisi.
Mwisho.
Mtoto Shauri John (wa pili kushoto) akiwa katika ya pamoja na wanafunzi wenzake shuleni kwao
0 Comments