Header Ads Widget

NCAA YASHAURIWA KUENDELEA KUBUNI MAZAO MAPYA YA UTALII MAPANGO YA AMBONI.

 

Na Matukio Daima Media,Tanga.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeishauri Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kuendelea kubuni mazao mapya ya utalii katika mapango ya Amboni yaliyopo mkoani Tanga ili kutoa fursa kwa wageni wengi zaidi kutembelea kivutio hicho urithi wa mambo kale.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii mheshimiwa Timotheo Mnzava ametoa maelekezo hayo kwa Wizara ya Maiasili na Utalii baada ya kumalizika kwa ziara ya wabunge wa kamati hiyo kuwa eneo hilo lina fursa nyingi la mazao mapya ya utalii hivyo ni jukumu la wizara na NCAA kukaa chini na kuona jinsi ya kuboresha mazingira ya mapango ya Amboni yawe ya kipekee na kuvutia zaidi.



“Ni jukumu lenu sasa kuhakikisha licha ya uwepo wa mapango haya lakini pia mnafanya kila jitihada kuwa na mazao mapya ya utalii kwa kuwa eneo hili ni kubwa na linaruhusu shughuli nyingi za utalii”, alisema Mhe.Mnzava.


Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii  Balozi Dkt. Pindi Chana aliwaeleza wabunge hao kuwa wizara yake itaendelea kusimamia maelekezo yote yanayotolewa na kamati ili kuhakikisha kuwa kila chanzo cha utalii kinachoanzishwa kinakuwa na tija kwa taifa.



Balozi Chana ameeleza kuwa wizara yake iliamua kukabidhi mapango hayo kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kuboresha uhifadhi, na kuyatangaza  zaidi ili kuongeza idadi ya watalii wa ndani na nje ya Nchi.


Naye Kamishna wa uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Dkt. Elirehema Doriye akizungumza mbele ya Wabunge hao alisema mamlaka imejipanga kuboresha eneo hilo kwa kuanzisha mazao mapya ya utalii ikiwemo makumbusho ya viumbe wa baharini, maeneo ya kupumzikia, mchezo wa kutembea na kamba “zip line” pamoja na huduma za nyingine za kijamii na kitalii katika eneo la mapango.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI