Header Ads Widget

MPLC YAPOKEA TUZO YA KUWAJENGEA UWEZO WANAWAKE


Na Lilian Kasenene, MorogoroMatukio DaimaApp 

Kituo cha Wasaidizi wa Kisheria Morogoro (MPLC), kimepokea tuzo ya kuwajengea uwezo wanawake wakulima wadogo katika kushiriki kwenye maswala ya uchumi kupitia wasaidizi wa kisheria katika wilaya za Malinyi,Kilombero na Ulanga.

Tuzo hiyo ilitolewa kwenye washa ya siku nne za kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu maswala ya jinsia na sera za usawa wa kijinsia.

Warsha hiyo iliwakutanisha wawakilishi wa mashirika 14 kutoka nchi 5 (Tanzania, Uganda, Kenya, Madagascar na msumbiji) yaliyokuwa yanatekeleza mradi wa kuimarisha usawa wa kijinsia kupitia taasisi za kiraia (Advancing Gender Equality Through Civil Society - AGECS),kwa ufadhili wa Aga Khani Foundation.

Katika utekelezaji wa mradi MPLC imetoa mafunzo kwa viongozi wa dini, mila, dawati la polisi na wajumbe wa baraza la kata kuhusu haki za mwanamke na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia. 

MPLC imetoa elimu ya kisheria na huduma za kisheria kupitia wasaidizi wa kisheria, jumla ya watu 15,885 wamefikiwa,wanawake 10754 na wanaume 5131.

Akizungumza kuhusu tuzo hiyo,Mkurugenzi wa Kituo cha Wasaidizi wa Kisheria Morogoro, Ndugu Amani Mwaipaja amewashukuru Aga Khan Foundation kwa mchango wao katika kuyajengea uwezo mashirika yasiyo ya kiserikali ili kuongeza ufanisi katika kuhudumia jamii.

Mwaipaja ametoa wito kwa wadau wa maendeleo (Development Partner) kuendele kujitokeza kufadhili miradi ya shirika hilo ili kuweza kuhudumia jamii ya kitanzania,kwa kuzingatia MPLC inategemea ufadhili na michango katika kutekeleza shughuli za shirika.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI