Header Ads Widget

MONGELA AONGOZA MAMIA KUAGA MIILI WALIOFARIKI AJALINI MBEYA


Naibu katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Tanzania bara John Mongela, ameongoza mamia ya waombolezaji jijini Mbeya kuaga miili ya watu wanne waliofariki kwa ajali ya gari akiwemo mwandishi wa habari wa kujitegemea Furaha Simchimba ajali iliyohusisha gari la Serikali na basi dogo mali ya kampuni ya CRN.

Akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mongela ameushukuru uongozi wa mkoa wa Mbeya kwa namna ambavyo wameshikamana katika kipindi hiki kigumu na juhudi ambazo zimefanyika katika kuokoa maisha ya majeruhi lakini pia kushirikiana katika hatua za kuwahifadhi ambao wamefariki.

Awali akizungumza kwenye zoezi la kuaga miili hiyo mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Mbeya Patrick Mwalunenge amesema kila mmoja anapaswa kujiandaa kwa kuwa hakuna anayeujua mwisho wake.

Naye spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson Mwansasu amewaomba waombolezaji kuelekeza maombi yao kwa majeruhi ambao wamelazwa wakiendelea na matibabu ili wapone haraka na kuendelea na majukumu yao.

February 25, 2025 ilitokea ajali ambayo ilihusisha magari mawili ambayo ni basi la kampuni ya CRN lenye namba za usajili T 599 DZQ linalofanya safari zake kati ya Mbeya na Mbarali na gari la serikali aina ya Toyota Landcruiser lenye namba za usajili STM 6167 mali ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mbeya baada kugongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya watu watatu papo hapo na kujeruhi wengine saba ambapo mwingine mmoja alifia hospitali.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI