Header Ads Widget

CCM DODOMA YAOMBWA KUINGILIA KATI MGOGORO WA ARDHI MAHOMANYIKA


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima app Dodoma

WAKAZI wa Mtaa wa Mahomanyika Jijini Dodoma wamekiomba chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma kuingilia kati katika suala lao la kuporwa ardhi, wakidai wanashinikizwa kuondoka kwenye maeneo yao kwa madai Wak kuvamia sehemu tengefu la serikali.

Wakizungumza na waandishi wa habari, wakazi hao, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mtaa, Abrahamu Mputu, wamesema wanaishangaa hali hiyo na kimya cha viongozi. 

“Tumeishi hapa kwa zaidi ya miaka 50, sasa tunashinikizwa na Jiji la Dodoma kwa kuwa tumeambiwa ni wavamizi wa maeneo yaliyotengwa,” amesisitiza Mputu.

Sarah Bwanakoo, mmoja wa wakazi hao, aliongeza kuwa ikiwa haki yao haitatolewa, watamtembelea Rais Samia Suluhu Hassan ili kutatua tatizo hilo.

 “Tutafika ofisi za CCM Mkoa kumueleza Mwenyekiti, Alhaj Omary Kimbisa, kuhusu malalamiko yetu. Lengo letu si kufanya fujo,” ameeleza.

Wakazi hao waliweza kifika  katika ofisi za CCM Mkoa lakini walikosa kumwona Kimbisa na badala yake walizungumza na Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Charles Mamba, ambaye aliahidi kutembelea eneo hilo.

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Dk. Fredrick Segamiko, hakupatikana kwa maoni baada ya kujaribu kumtafuta kwa simu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI