Header Ads Widget

MAGARI CHAKAVU YAKWAMISHA UKATAJI BIMA ZA MAGARI

 

Dk.Baghayo Saqware Kamishna wa TIRA nchini
Hassan Rugwa RAS Kigoma

Meneja wa TIRA kanda ya ziwa Tanganyika

Na Fadhili Abdallah

Mamlaka ya usimamizi wa bima nchini (TIRA) imesema kuwa magari chakavu yanayotaka kukatiwa bima imekuwa kikwazo kikubwa kwa taasisi hiyo katika kukubaliana na matakwa ya wamiliki wa magari hayo kukatiwa bima.

Kamishna wa TIRA Dk. Baghayo Saqware

 alitoa kauli hiyo katika mkutano na watumishi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa Kigoma akitoa elimu ya umuhimu wa bima kwa jamii kwa ajili ya kuhamasisha ukataji wa bima za mali,afya na vyombo vya moto.

Saqware alisema kuwa wamekuwa wakipata wakati mgumu kukubali kuyakatia bima baadhi ya magari ambayo yamekuwa na uchakavu mkubwa ambayo kwa mujibu wa sheria na taratibu za bima hazikidhi vigezo vya kukatiwa bima.

Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi Bima wa kanda ya ziwa Tanganyika, Kulenje Mbura

Pamoja na hilo  amewahamasisha viongozi na  wananchi wa mkoa Kigoma kuwekeza zaidi katika uanzishaji wa ofisi zinazotoa huduma za  bima kwani mkoa wa kigoma bado uko nyuma 1kwa wananchi wake kukata bima licha ya kuwa na biashara nyingi na  kubwa zinazopaswa kukatiwa bima.

Akifungua Mkutano huo Katibu tawala wa mkoa wa Kigoma, Hassan Rugwa amewataka watendaji katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kigoma kutumia elimu  ya umuhimu wa Bima walioipata kuiepeleka kwa jamii ili  kubadili mtazamo wa  jamii katika kutambua umuhimu wa bima na kukata bima mbalimbali kwa ajili ya maisha yao.

Sambamba na hilo Katibu Tawala huyo wa mkoa Kigoma ameitaka TIRA kufanya mapitio ili kujua kuna uhitaji kiasi gani ili serikali ya mkoa iongeze nguvu katika kuhakikisha jamii ya mkoa wa Kigoma inafikiwa na elimu ya Bima ili waweze kuokoa maisha ya watu na Mali zao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI