Na Hamida Ramadhan matukio Daima App Dodoma
MFUKO wa Utamaduni na Sanaa Tanzania umetoa mikopo yenye thamani ya shilingi 1,246,215,189 kwa miradi ya 78 ya muziki ambapo kiasi hicho kwa wasanii lengo likiwa ni kuwawezesha
Kununua vifaa vya kisasa kwa studio 42 za kuzalishia muziki .
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania, Nyakaho Mahemba,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita leo tarehe 28 Februari, 2025, katika ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, Dodoma.
Amesema uwepo wa studio hizo umesaidia kuondoa adha na gharama kwa wanamuziki kuzalishia kazi zao nje ya nchi.
Amesema Studio hizo za kisasa zimewahamasisha wasanii mbalimbali kutoka nje ya nchi kuja nchini kwetu kwa ajili ya kuzalisha kazi zao.
Hata hivyo amesema studio hizo zimekuwa ni chanzo cha mapato ya fedha za kigeni na kuongeza ujuzi, kubadilishana uzoefu na wasanii nchini.
" Fedha hizo pia zimetumika kununua vifaa vya kisasa kwa bendi 18 za muziki wa injili, bendi 13 za muziki wa dansi na Bendi 3 za muziki wa Taarabu Kuendesha matamasha 16 ya muziki wa nyimbo za injili yaliyoshirikisha wasanii wa ndani na nje ya nchi, matamasha 18 ya muziki wa nyimbo za Singeli yaliyoibua vipaji vipya kwa wasanii 117," Amesema
Na kuongeza" Kutengeza jumla ya nyimbo za Audio 124 na video 36;
Kununua majukwaa ya kisasa matatu (3) kwa ajili ya kazi za Sanaa
Kuwezesha Chuo kimoja cha UD-J ambacho kimezalisha ma- DJ 288 ambapo wengi wao wameajiriwa katika Vituo vya Redio, Luninga, Kumbi za Burudani na Starehe na wengine wamefanikiwa kujiajiri wenyewe, " Amesema Mahemba
Kwa upande wa Sekta la Filamu
Mfuko umetoa mikopo yenye thamani ya shilingi 1,329,007,342.00 kwa miradi 90 na kuwezesha kununua vifaa vya kisasa kwa Studio 61 za kuzalishia filamu na tamthiliya ambapo vifaa hivyo vimeongeza ubora na mwonekano wa kazi hivyo kuzifanya kukubalika ndani na nje ya nchi.
Pia fedha hizo zimeweza Kuboresha mandhari/mwonekano wa Ofisi za Studio 9; Kuzalisha filamu 241, tamthiliya 9 zinazorushwa katika vituo mbalimbali vya habari pamoja na mitandao ya kijamii Umekuwa kichocheo kwa wasanii wa nje ya nchi kushirikiana na wasanii wa ndani ikiwa pamoja na kutumia vifaa vya uzalishaji vya kisasa vilivyowezeshwa na Mfuko.
"Fedha hizo kupitia Mfuko wa Utamaduni Umewezesha kukarabati Ofisi kwa Maktaba za Video 11 na ununuzi laptop za kisasa 6 , "Amesema Mahemba
Mwisho
0 Comments