Header Ads Widget

MAPUNGUFU YA NYARAKA KWENYE MIRADI YANAJENGA HOFU YA UBADHIRIFU - TAKUKURU

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

TAASISI  ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa Kigoma imesema kuwa mapungufu makubwa kwenye nyaraka za manunuzi ya miradi na nyaraka za kupokea vifaa na fedha mkoani humo imekuwa changamoto kubwa ambayo wahusika wanalenga kupoteza ushahidi wa ubadhirifu kwenye miradi.

NAIBU Mkuu wa  TAKUKURU Mkoa wa Kigoma,  John Mgallah amesema hayo akitoa taarifa kwa waandishi wahabari kuhusu utendaji wa taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu katika kuchunguza miradi mbalimbali  inayoendelea mkoani humo.

Katika uchunguzi huo TAKUKURU imepitia na kuchunguza miradi 31 yenye thamani ya shilingi Bilioni 11.4 ambapo miradi hiyo imekutwa na mapungufu mbalimbali ikiwemo kutoonekana vitabu vya stoo vya kupokea na kutoa vifaa, kutokuwepo kwa ramani za ujenzi

Mgallah akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa Habari alitoa mfano wa  ujenzi wa  ya shule  moja ya Msingi katika wilaya ya Uvinza ambayo kwa sasa anahifadhi jina ambayo imeonekana kuwa na changamoto ya utekelezaji wake ambapo kiasi cha shilingi milioni 100 zimepelekwa shuleni hapo ambapo kwa sasa uchunguzi kuhusu mradi huo umeanza.

Aidha Naibu Mkuu huyo wa TAKUKURU mkoa Kigoma alitaja maeneo mengine kuwa ni Halmashauri ya wilaya ya Kigoma ambapo shule ya sekondari Nyarubanda ambapo kuna ujenzi wa bweni moja, madarasa matatu  na matundu sita ya vyoo mradi huo ulikumbwa na mapungufu mbalimbali ikiwemo kutoonekana daftari la kutunzia vifaa.

Sambamba na shule hiyo pia shule ya Msingi Nyarubanda  katika  Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma inayotekeleza mradi wa madarasa mawili na matundu nane ya vyoo  pia mradi huo ulikumbwa changamoto na mapungufu mengi ambayo yanatia shika uadilifu na kusihindwa kufuata taratibu katika usimamizi wa miradi hiyo

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI