Header Ads Widget

GAVANA BWANKU ATEMBELEA KYANYABASA PANAPOJENGWA DARAJA LA KISASA PALIPOTESA WANANCHI WA BUKOBA MIAKA MINGI, RAIS SAMIA ATOA BILIONI 9.7



Afisa Tarafa wa Tarafa ya Katerero, Ndugu Bwanku M Bwanku ametembelea kuona Ujenzi wa daraja kwenye Kivuko cha Kyanyabasa linalounganisha Kata za Bujugo na Kishogo za Tarafa ya Katerero na Wilaya nzima ya Bukoba na kukuta Mkandarasi Kampuni ya Gemen Engineering akiwa site na mitambo mikubwa, malori zaidi ya 5 yakiendelea kumwaga vifusi ndani ya Mto kuelekea ujenzi wa daraja hilo la kisasa.


Gavana Bwanku amebainisha kuwa, Eneo hilo limekuwa  linawatesa Wananchi miaka kwa miaka, lakini sasa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa Bilioni 9.7 kujenga daraja hilo la kisasa kukatisha Mto Ngono na kuondoa usafiri wa mitumbwi na Kivuko.


"Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha kujengwa daraja hili kiasi cha BILIONI 9.7. Amesikia kero za  Wananchi walikua wanalipia fedha kuvuka tena ikifika usiku Kivuko kinafungwa.

Kwa sasa kila mwana Bukoba, anasema huu ni ukombozi na hakuna aliyeamini lakini Rais Samia amefanikisha hili." Amesema Gavana Bwanku.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI