Header Ads Widget

MALIASILI NA UTALII MNATAFSIRI MAONO YA MHE. RAIS KWA VITENDO-MHE. VUMA

 


Na. Anangisye Mwateba-Makuyuni Arusha


Wizara ya maliasili na utalii imepongezwa kwa kutafsiri  kwa vitendo maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuonyesha  juhudi kubwa katika kuendeleza sekta ya utalii kwa kufanya uwekezaji mkubwa kwenye Taasisi za wizara ikiwemo Mamlaka ya usimamizi wa Wanyapori Tanzania (TAWA).


Pongezi hizo zimetolewa  na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, Mhe. Vuma Augustine Holle wakati wa kuhitimisha ziara ya ukaguzi wa Miradi inayotekelezwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori katika (TAWA) katika Hifadhi ya wanyamapori Makuyuni.


Mhe. Vuma aliongeza kuwa iko haja kwa Taasisi zilizokabidhiwa maeneo yaliyotaifishwa na serikali kuja kujifunza katika eneo la Hifadhi ya wanyamapori Makuyuni  juu ya  uwekezaji na uendelezaji  uliofanywa na TAWA kwa kipindi kifupi baada ya kukabidhiwa eneo hilo kutoka kwa Msajili wa Hazina.


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma imefanya ziara katika hifadhi ya Wanyamapori Makuyuni kwa lengo la kukagua utelezaji wa miradi na uendelezaji wa eneo hilo baada ya kukabidhiwa kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kutoka kwa Msajili wa Hazina baada ya kutaifishwa kutoka  kampuni ya Rift Valley Seed Company Limited,


Baada ya kukabiidhiwa eneo hilo, TAWA walilifanya kuwa Hifadhi ya Wanyamapori na kuwekeza katika kuboresha miundombinu ili kuvutia watalii ambapo tangu likabidhiwe mwezi machi 2023, idadi ya watalii waliotembelea imeongezeka kutoka 291 mwaka 2023/24 hadi 405 kwa kipindi cha Julai 2024 – Januari 2025; lakini pia ukusanyaji wa mapato uliongezeka  kutoka Shilingi 14,535,832.08 mwaka 2023/24 hadi Shilingi 251,655,828.28 katika kipindi cha Julai 2024 hadi Januari 2025.


Naibu Waziri Maliasili na Utalii, Mhe Dunstan Kitandula  aliishukuru kamati kwa kuona umuhimu wa kuja kuona kwa uhalisia uendelezaji na  uwekezaji mkubwa unaondelea kufanywa na wizara kupitia TAWA, Vilevile alisema kuwa muonekano wa eneo hilo kwa sasa ni maono ya Mhe. Rais katika kuendeleza sekta ya utalii lakini pia ni ushauri unaotolewa na wabunge kupitia  michango yao mbalimbali katika Sekta ya Uhifadhi na Utalii. 


Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Meja Jenerali Mstaafu, Hamis Semfuko alisema kuwa wanatarajia kufanya uwekezaji mkubwa na wakipekee ambao utaendana na tamaduni za kitanzania ikiwemo Kujenga Hoteli katika eneo la kupokelea wageni itakayokuwa inapika  vyakula vya asili tu.










Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI