Na Costa Sakagoi- Matukio Daima App, SIMIYU.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesisitiza matumizi ya Nishati Safi kwenye Taasisi za Umma na Mashuleni zinazohudumia zaidi ya watu 100 na kuendelea.
Ameyasema hayo leo Feb 16, 2025 katika Jimbo la Maswa Mashariki aliposhiriki Mkutano Mkuu wa dharura kwa ajili ya kuwalisilisha Utekelezaji wa Ilani ya CCM, huku akisisitiza kuwa walitangaza kufikia mwezi wa 12 mwaka jana, Taasisi zote kutumia nashati safi ya kupikia.
Ameeleza kuwa awali taasisi hizo ziliomba zipitishe kwanza Bajeti ili ziweze kutekeleza Mpango huo ambapo Waziri Majaliwa amesema kuwa serikali imewaongezea miezi mitano hadi mwezi Juni ili waanze kupikia Nishati Safi kwenye Taasisi za Umma na binafsi.
Katika hatua nyingine, Majaliwa amesisitiza kupiga marufuku michango mashuleni ambayo haijapitishwa na Mkuu wa Wilaya huku akiwasisitiza wazazi kupeleka watoto Shule.
"Tunazuia na kupiga marufuku michango ya hovyohovyo mashuleni isipokuwa ile inayosimamiwa na Wakuu wa Wilaya...siyo kila mmoja aibuke kuchangisha michango, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara za Elimu simamieni maelekezo haya" amesema.
0 Comments