MATUKIO DAIMA
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa Leo Februari,02,2025 imepitisha Rasimu ya bajeti ya RUWASA,TARURA na TANESCO kwa ajili ya uendeshaji wa Shughuli mbalimbali za Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Bajeti iliyolenga kuboresha huduma za kijamii,miundombinu na maendeleo ya kiuchumi.
Hayo yamesemwa wakati wa kupokea na kujadili taarifa ya robo ya pili ya mwaka wa fedha 2024/2025 kwa taasisi za kiserikali kwenye kikao cha baraza la madiwani ndipo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Nkasi Mhe, Pancras Maliyatabu amewapongeza wataalamu kwa kuandaa Rasimu vizuri huku akiwataka wakala wa barabara za vijijini na mjini (TARURA) kutenga bajeti ya dharura ili kuweza Kurekebisha miundombinu ya barabara itakayokatika wakati wa mvua pamoja na kuthibiti wananchi kuacha tabia ya kulima kandokando mwa barabara ili kuepuka mmonyoko wa udongo.
Mhandisi Lumala Madirisha kaimu Meneja Wilaya ya Nkasi wa wakala wa barabara za vijijini na mjini (TARURA) amewasilisha Rasimu ya Mpango wa Bajeti ya barabara kutoka vyanzo mbalimbali ambayo inazaidi ya Bilioni nne (4,061,390,000.000) yenye lengo la kuboresha na kujenga barabara katika Mji wa Mafinga ambapo kwa pamoja Madiwani waliipitisha.
Thomas petro fundi sanifu RUWASA ameeleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2025/2026 wilaya ya nkasi itaendelea na ukamilishaji wa miradi mitano (5) ambayo haitakamilika katika mwaka huu wa fedha aidha kutokana na kuchelewa kwa fedha sanjari na kuanza ujenzi wa miradi mipya nane (8),miradi mitatu (3) kupitia fedha za wafadhili P4R na miradi mitano (5) kupitia program ya maji na usafi wa mazingira (MUM).
Nae meneja wa Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) wilaya ya Nkasi Mhandisi Henry Frimin ameeleza kuwa miradi mipya inayoenda kutekelezwa katika Halmashauri ya Nkasi kwa Mwaka wa fedha 2025/2026 ikiwa ni mwai KM 9 LT,Ipanda mkole 4KM,Msilihofu 3KM,Wampembe 2KM, Nkasi 6KM,Lyele-Swaila KM.
Kikao cha Baraza la madiwani la kujadili mpango na Bajeti 2025/2026 limehudhuliwa na kaimu katibu tawala wa wilaya,Mbunge,Madiwani,wakuu wa idara na vitengo pamoja na Watendaji wa kata.
0 Comments