Header Ads Widget

MFUMO WA ANWANI ZA MAKAZI NI ENDELEVU

 


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App Dodoma


WAZIRI wa Habari Mawasilino na Teknolojia ya Habari Jerry Silaa amesema kuwa Utekelezaji wa Mfumo wa Anwani za Makazi ni endelevu kutokana na mabadiliko ya makazi, wakazi, na huduma. 


Amebainisha hayo leo jijini Dodoma wakati akifungua maadhimishoya wiki ya Anwani za makazi huku akieleza kuwa, shughuli mbalimbali za Mfumo zinaendelea kutekelezwa ikiwemo kukusanya, kuhakiki na kuhuisha taarifa za Anwani za Makazi. 



kuboresha utendaji kazi wa Mfumo wa NaPA; Amesema wataendelea kutoa elimu kwa umma na kuhamasisha utekelezaji, uendelezaji na matumizi ya Mfumo wa Anwani za Makazi. 


"Katika kuendeleza jitihada zilizoanzishwa kupitia Operesheni tajwa, Serikali imeona ni vyema kuwa na Maadhimisho ya Wiki ya Anwani za Makazi yatakayokuwa yanafanyika kila mwaka, " Amesema



Na kuongeza " Kufanyika kwa Maadhimisho hayo kutaongeza hamasa kwa Taasisi za umma na Binafsi pamoja na Wananchi kuweza kutambua na kutumia Anwani za Makazi katika shughuli za kijamii na kiuchumi," 



"Vilevile, maadhimisho haya, yanatarajiwa kuongeza kasi ya utekelezaji na matumizi endelevu ya Mfumo wa Anwani za Makazi, " Amesema.



Aidha amesema Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa kila nyumba, jengo, kiwanja, huduma, ofisi ama eneo la biashara linatambulika kwa Anwani ya Makazi ambapo Anwani ya Makazi inaundwa na Namba ya Anwani maarufu kama namba ya nyumba; Jina la Barabara au Mtaa; na Postikodi.


 Postikodi ama nchi zingine zinaita Zipcode ni utaalamu wa kugawa maeneo ili kurahisisha utambuzi. 



"Kwa hapa Tanzania mgawanyo huu umefanyika katika ngazi ya kata ambapo kila Kata ina Postikodi yake yenye tarakimu tano, " Amesema 


Ameeleza Anwani za Makazi inarahisisha utoaji na upokeaji wa huduma mbalimbali ili kuchochea maendeleo ya Kiuchumi na kijamii hasa katika zama hizi ambazo Mapinduzi ya 4,5 na 6 ya viwanda yanategemea matumizi ya TEHAMA. 



"Na matumizi ya TEHAMA yanalazimu kuwa na mifumo ya utambuzi ndiyo sababu ya Serikali kuanzia mfumo huu, " . 


Amesema Mfumo wa Anwani za Makazi ni nyenzo ya utambuzi ambayo inatambulisha wakazi na makazi na uwepo wa mfumo huu kwa upande wa OR-TAMISEMI ni nyenzo muhimu zaidi kwani kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Serikali za Mitaa, jukumu la kutoa majina ya mitaa lipo OR-TAMISEMI, hivyo utekelezaji wa mfumo huu unarahisisha utekelezaji wa jukumu la kutoa majina ya mitaa kama ambavyo kauli mbiu ya maadhimisho haya inavyosema TAMBUA NA TUMIA ANWANI ZA KAZI KURAHISISHA UTOAJI NA UPOKEAJI WA HUDUMA. 



Akiongea kwa niaba ya Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais TAMISEMI Mohamed M Chengerwa Naibu Wziri wa TAMISEMI Festo Ndugange Amesema TAMISEMI ni mdau mkuu katika utekelezaji hususan kupitia kwa Watendaji wa Kata, Vijiji na Mitaa ambao wana wajibu wa kuwezesha uwekaji wa miundombinu; kuhuisha taarifa; na kukusanya taarifa mpya.



 "TAMISEMI ni mnufaika mkubwa katika matumizi ya Mfumo; hii ni kwa kuzingatia kwamba Mfumo unawezesha utambuzi hivyo hurahisisha utoaji na upokeaji wa huduma. ," Amesema 


Na kuongeza "TAMISEMI ndiyo yenye wananchi na ndiyo mtoa huduma mkuu kwa wananchi, hivyo TAMISEMI inauhitaji sana Mfumo huu na kwa sasa tulifanya majaribio ya kutoa barua kwa njia ya kidijitali ambapo jambo hilo limeonyesha kuwa la mafanikio.

 

Hata hivyo kilele cha Maadhimisho haya kitafanyika tarehe 8 Februari, 2025 ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI