Header Ads Widget

MCHANGO WA SEKTA YA BANDARI TRILIONI 10 . 8 MWAKA WA FEDHA 2022/23


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App Dodoma 

KATIKA mwaka wa fedha wa 2022/23 mchango wa sekta ya bandari ulikuwa Shilingi trilioni 10.8 sawa na asilimia 7.3 ya pato la Taifa lililokuwa Shilingi trilioni 148.3 huku akibainishwa kuwa Ongezeko hilo la mapato limetokana na Mapato ya matumizi ya bandari (wharfage charges) kuongezeka kutokana na ongezeko la shehena iliyohudumiwa bandarini Mapato ya kuhudumia meli (marine charges). 

Akiongea na waandishi wa habari February 24 jijini Dodoma wakati akieleza mafanikio ya serikali ya awamu ya Sita Mkurugenzi  Mkuu Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari 

Tanzania TPA Plasduce  Mbossa amesema Mapato hayo yameongezaka kutokana na ongezeko la idadi ya meli na ukubwa wa meli Mapato ya mrabaha (royalty) kwa tani au kasha linalohudumiwa na Kampuni ya DPW Dar es Salaam na Tanzania East Africa Gateway Terminal Limited (TEGTL) pamoja na tozo la pango (Lease Rent) la maeneo ya bandari iliyolipwa na kampuni hizo kwenda Serikalini kupitia TPA.

Amesema Katika kipindi cha miezi sita ya Mwaka wa Fedha 2024/25 (Julai-Desemba, 2024), jumla ya Shehena iliyohudumiwa na Bandari za TPA ni tani milioni 15.49 ambayo imezidi lengo lililowekwa la kuhudumia tani milioni 14.60 kwa asilimia 6.1,  ikiwa  ni sawa na ongezeko la asilimia 11.1 ikilinganishwa na tani milioni  13.94 iliyohudumiwa kipindi kama hiki mwaka uliopita (Julai-Desemba, 2023).  

Aidha amesema, jumla ya Shehena ya Makasha iliyohudumiwa na Bandari za TPA ni Makasha TEUS 565,361, ikiwa  ni sawa na ongezeko la asilimia 4.9 ikilinganishwa na shehena ya Makasha TEUS 539,013 iliyohudumiwa kipindi kama hiki mwaka uliopita (Julai-Desemba, 2023).

"Pamoja na utendaji kazi mzuri ulioainishwa hapo juu bado sekta ndogo ya bandari inakabiliwa na changamoto kuu zifuatazo:Uchache wa gati zinazoweza kukidhi ongezeko la idadi na ukubwa wa meli.Uchakavu wa miundombinu ya bandari na isiyokidhi mahitaji ya meli za kisasa Ufinyu wa maeneo ya kuhudumia na kuhifadhi shehena, " Amesema Mbossa

AmesemaUkosefu wa rasilimali fedha kwa ajili ya uendelezaji wa miundombinu Miundombinu wezeshi (barabara na reli) isiyokidhi mahitaji ya ukuaji wa shehena Meli zingine kuamua kwenda bandari shindani kutokana na changamoto za muda wa huduma na ufanisi.Ukosefu wa meli na vyombo vya kisasa vya usafiri wa maji.

Mabadiliko ya tabia nchi yanayoathiri operesheni katika bandari zetu za maziwa.

Amesema Katika kukabiliana na changamoto zilizoainishwa hapo awali, serikali ya awamu ya sita kupitia TPA imefanya yafuatayo Ununuzi wa Mitambo Hadi kufikia mwezi Februari 2025, TPA imenunua na imepokea vitendea kazi kama ifuatavyo

Reach Stakers’ saba (7), ‘Pilot Boats’ tatu (3), ‘All Terrain Mobile Crane’ moja (1), Forklifts sabini na tisa (79) kwa ajili Bandari za DSM, Ziwa Victoria na Kigoma, Cranes tano (5) za kisasa (SSG) za kupakia na kushusha makasha Bandarini kwa ajili ya Bandari ya DSM na Mtwara(Crane zingine mbili (2) zinatarajiwa kupokelewa kabla ya mwezi Juni, 2025), Tug Boat sita (6) kwa ajili ya Bandari ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara, Boat mbili (2) za ukaguzi ziwa Nyasa na ziwa Tanganyika.

Shughuli za uendeshaji wa Kitengo  cha Bandari ya Dar es Salaam gati. 

Amesema Kampuni ya DP World Dar es Salaam inaendelea na utekelezaji wa Mpango wa Uwekezaji ambao unakusudiwa kugharimu kiasi cha Dola za Marekani (USD) 250 Milioni (sawa na shilingi za Tanzania Bilioni 675) kwa kipindi cha awali cha Mkataba cha Miaka mitano (5). 

"Hadi sasa, Kampuni ya DP World imefanya uwekezaji wa awali katika maeneo mbalimbali ya uendeshaji ili kuboresha na kuongeza ufanisi wa huduma za bandari ambalo ni dhumuni kuu la kuingiwa kwa Mikataba kama ilivyoelezwa hapo awali Uwekezaji wa awali uliogharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 214.42 umefanywa katika maeneo mbalimbali ikiwemo, " Amesema Mbossa

Ameeleza Ununuzi na usimikaji wa mitambo krini za kisasa (Ship to Shore Gantry Cranes) za kuhudumiwa shehena ya makasha uliogharimu Shilingi Bilioni 115.80. Ununuzi na usimikaji wa mitambo nane (8) inayotambulika kama “Rubber Tyred Gantry Crane-RTG” katika Gati Na. 1 la makasha la Bandari ya Dar es Salaam iliogharimu kiasi cha shilingi bilioni 96;

Ununuzi wa ‘terminal tractors’ ishirini (20) ambazo hutumika katika kuhamisha na kusafirisha shehena kutoka eneo moja la bandari kwenda eneo jingine na ‘trailer’ thelathini na moja (31) ambazo hutumika katika kubeba shehena za aina mbalimbali vilivyogharimu Shilingi Bilioni 13.32; 

na Kusanifu na kusimika mfumo wa kisasa wa TEHAMA wa kuhudumia shehena ambao kitaalamu hutambulika kama ‘Terminal Operating System’ ambao ni mahususi kwa kutoa huduma za uendeshaji wa bandari ambao umegharimu Shilingi Bilioni 3.6.

Amesema Shughuli za Uendeshaji wa Kitengo Na. 2 cha Bandari ya Dar es Salaam gati Katika kuhakikisha Bandari ya Dar es Salaam inafanya kazi kwa ufanisi na tija, Serikali kupitia TPA iliingia mikataba ya ushirikishaji wa sekta binafsi kwa ajili ya kuendesha Bandari ya Dar es Salaam.

Ameeleza Shughuli za uendeshaji wa Kitengo Na. 2 cha Bandari ya Dar es Salaam zilikabidhiwa rasmi kwa kampuni ya East Africa Gateway Terminal Limited – TEGTL mwezi Julai 2024.

 "Utekelezaji wa Mpango wa UwekezajiKampuni ya Tanzania East Africa Gateway Limited (TEAGTL) inaendelea na utekelezaji wa Mpango wa Uwekezaji ambao unakusudiwa kugharimu kiasi cha Dola za Marekani (USD) 495 Milioni (sawa na Shilingi za Tanzania Trilioni 1.337) kwa kipindi cha awali cha Mkataba cha Miaka Thelathini (30)," Amesema. 

 Manufaa Mtambuka ya Ushirikishaji wa Sekta Binafsi katika Bandari ya Dar es Salaam

Amesema Mapato ya Kodi ya Forodha yameimarika kwa ufanisi na uendeshaji wa shughuli za Bandari ya Dar es Salaam kufuatia maboresho yaliyofanywa na DP World kumechagiza pia makusanyo ya mapato ya Serikali hususani yale yanayotokana na kodi. 

Hali hiyo imepelekea Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuongeza makusanyo hadi kufikia wastani wa shilingi Trilioni moja (1) kwa mwezi kwa mwaka 2024/25 kutoka wastani wa Shilingi Bilioni 850 kwa kipindi cha mwaka 2023/24.

Kupungua kwa Msongamano wa Meli na Gharama za Usafirishaji wa Shehena Katika kipindi kinachoanzia mwezi Septemba 2024 hadi Novemba 2024 ambacho ndicho kipindi cha msimu wa meli na shehena nyingi (peak season) inayoingia nchini na kusafirishwa kwenda nje ya nchi. 

Kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha zaidi ya miaka mitatu (3), Bandari ya Dar es Salaam imeweza kuhudumia shehena mbalimbali zinazosafirishwa na wafanyabiashara kwa ajili ya biashara za mwisho wa mwaka bila ya kuwepo kwa malalamiko ya kucheleweshwa kwa shehena hizo. 

Hali kadhalika, baadhi ya makampuni ya meli yameanza kupunguza gharama za usafirishaji wa shehena kwa njia ya maji kufuatia kuondoshwa kwa muda kusubiri nangani kwa meli za makasha. 

"Kwa mfano, Kampuni ya MSC imeondosha kiasi cha Dola za Marekani (USD) 1,000 kwa kasha ambacho kilikuwa kikitozwa kama tozo ya ziada kwa mteja kwa sababu ya ucheleweshaji wa uhudumiaji wa makasha katika Bandari ya Dar es Salaam, " 

Na Kuongeza "Kuondolewa kwa tozo hii kumetoa nafuu kwa watumiaji wa bandari katika usafirishaji wa shehena kupitia bandari Ajira kwa Wazawa katika Kampuni za WawekezajiKatika kipindi cha kuanzia Aprili 2024 hadi Januari 2025, jumla ya wafanyakazi 779 wenye fani mbalimbali wamepata ajira za moja kwa moja kwenye kampuni zinazoendesha Kitengo Na. 1 na Kitengo Na. 2 vya Bandari ya Dar es Salaam. 

Amesema kati ya hao wafanyakazi  299 wameajiriwa katika Kampuni ya DP World Dar es Salaam na wafanyakazi 480 wameajiriwa katika kampuni ya  TAEGTL.

Amesema hivi sasa Serikali ya Awamu ya Sita kupitia TPA inaendelea kutekeleza mapendekezo ya mpango kabambe ya maendeleo ya bandari nchini (2020 – 2045) na programu ya uboreshaji na uendeshaji wa bandari ambao ni mpango wa kitaifa (National Projects Management Information System – NPMIS) ambayo ilisajiliwa Oktoba, 2023 kwa jina la Tanzania Ports Development and Management Programme na kupewa namba ya mradi 4300.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI