Na Lilian Kasenene, Morogoro, Matukio DaimaApp.
FESTO Francis Makambula(34) mkulima na mkazi wa kijiji ccha Mululu wilaya ya Kilosa anashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa Morogoro kwa tuhuma za kumuua Rashid Bandei Kiupi(49)mlinzi wa kampuni ya Stigmaltin baada ya kumvamia na kumshambulia kisha kumchoma kisu kifuani na kusababisha kifo chake.
Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro Alex Mkama akizungumza na waandishi wa habari alisema tukio hilo limetokea Februari 18, 2025 majira ya asubuhi huko katika eneo la Mululu Kisanga ambapo mtuhumiwa alimshambulia mrehemu wakati anakwenda kazini.
Mkama alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni ugomvi unaohusiana na mahusiano ya mapenzi kati ya marehemu na dada yake mtuhumiwa, na kwamba hatua za upelelezi zinakamilishwa ili mtuhumiwa afikishwe kwenye vyombo vya vingine katika mnyororo wa haki jinai.
Katika tukio lingine, kamanda Mkama alimtaja Philibert Mtamiela(52)mkulima na mkazi wa kijiji cha Tangihuru wilaya ya Malinyi ambaye alikutwa amekuf kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya viatu akiwa ndani ya kibanda kinachotumiwa kwa shughuli za shamba.
Alisema tukio hilo lilitokea Februaru 19,2025 hulko Malinyi ambapo awali marehemu alikuwa akitafutwa kwa tuhuma za tukio la kumuua mke wake kwa kutumia silaha nyenye makali sehemu ya kichwani.
Kamanda huyo alisema mume huyo baada ya kuhakikisha amemuua alipiga simu kwa ndugu mbalimbali akiwafahamisha kuwa amemuua mkewe kwa sababu amechoshwa na matatizo mbalimbali aliyokuwa akiyafanya mkewe huyo marehemu.






0 Comments