Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi.
Na Hamida Ramadhan matukio Daima App Dodoma
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt Emmanuel Nchimbi amekuwa mbogo kwa Makada wanaofanya sherehe binafsi kwa kivuli cha chama na kuwataka kuacha Mara moja kwani ni kinyume cha utaratibu wa chama hicho.
Hayo ameyasema leo February 19 jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya Watendaji wa Kata na Makatibu Tawi wa Mkoa wa Dodoma .
Amesema katika siku za hivi karibuni kumezuka utaratibu kwa baadhi ya makada wa CCM kutengeneza matukio ya kumbumizi za kuzaliwa,kumbikizi za ndoa na kuwaalika wanachama na kuwalipa posho.
"Niseme wazi chama Cha Mapinduzi CCM kinamfumo wake wa kufuatilia kila kinachotokea na kumbukumbu hizi tunazokusanya ndizo zitakazowaengua au kuwatoa kwenye kugombea, " Amesema Dkt
Aidha akielezea mafunzo hayo amesema
ni maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt Samia Suluhu Hassan lengo likiwa ni kuwa na watendaji wanaotambua wajibu wao .
" Mafunzo haya yanakwenda kuwakumbusha majukumu yenu kama watendaji wa chama na jinsi gani tutashinda kwa kishindo uchaguzi mkubwa wa Rais, Wabunge na Madiwani, " Amesema
Na kuongeza " Hii iko wazi lengo kuu la chama chochote cha siasi ni kushika dola hivyo kwa upande wetu dola tumeshika kikubwa ni kushinda kwa kishindo kwani kushindwa kwa chama ni kunatokana na wanachama husika na kushinda kwa chama kunategemea wanachama hivyo tukawe waadilifu, " Amesema
Kwa upande wake Katibu NEC Organization Issa Haji Gavu amesema mafunzo hayo ni maelekezo ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na kusimamiwa na Katibu Mkuu Dkt Nchimbi.
"Kwanini mafunzo haya kwa watendaji hawa ni kwasababu chama kipo na kinaanzia kwenye ngazi ya Shina hadi Taifa hivyo niwaombe muwe wasikivu na kuzingatia mnavyoelekezwa, " Amesema Gavu.
Naye Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Dodoma Pili Mbaga amesema mafunzo hayo kwa watendaji wa Kata na Matawi yanakwenda kuwajenga kwani wapo nyuma ya muda na mafunzo haya yataleta muongozo .
Mwisho.
0 Comments