Watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ngazi ya mkoa, mkoani Lindi, wamekula kiapo cha uadilifu na kujitoa kujito au kuthibitisha kutokuwa mwanachama wa chama cha siasa ikiwa ni maandalizi ya kuanza rasm zoezi la uandikishaji huo January 28 mwaka huu Katika Mkoa huo .
wamekula kiapo hicho Leo January 17,2025 mbele ya hakimu Mkazi Mkuu Mfawidi Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Consolata Singano Katika ukumbi wa Mkutano ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi mjini hapo wakihudishwa mratibu wa uandikishaji wa Mkoa , maafisa uandikishaji, maafisa uandikishaji wasaidizi Ngazi ya Jimbo, maafisa Uchaguzi , maafisa ugavi na maafisa tehama wa Halmashauri .
Mheshimiwa Singano Amesema Katika kutekeleza shughuli za uchaguzi kunakuwa na mambo mengi ambayo mengine ni Siri na na mengine yanakuwa ni ya Siri kwa muda mpaka pale Uchaguzi utakapokamilika hivyo ni muhimu kabisa Watendaji hao Kula kiapo hicho.
Mheshimiwa Singano amefafanua kuwa Hata Sheria ya usalama wa Taifa inayosimamia viapo imeelekeza wazi kwamba ukikiuka kiapo ulichoapa kuna adhabu zake na ukizingatia unyeti wa zoezi hilo la Uchaguzi .
Kiapo hicho kilienda sambamba na utoaji wa Mafunzo kwa Watendaji hao kuhusu uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura yakihusisha namna ya ujazaji wa fomu pamoja na kutumia mfumo wa kuandikisha Wapiga Kura( Votes Registration system) kwa lengo la kuwapa uelewa wa pamoja utakaowapa fursa ya kutumia kwa ufasaha Mfumo huo pamoja na vifaa vingine vya kuandikisha Wapiga Kura .
Akifungua Mafunzo hayo Makamu Mwenyekiti wa tume huru ya Taifa ya uchaguzi Jaji msahafu Mbarouk Mbarouk alisema Mafunzo hayo ni mahususi kwa ajili ya kuwajengea umahiri wa kuwafundisha maafisa waandikishaji Ngazi ya Kata ambao watatoa Mafunzo kwa waendeshaji wa vifaa vya Bayometriki na waandishi wasaidizi watakaohusika na uandikishaji wa Wapiga Kura vituoni.
Hata hivyo Jaji msahafu Mbarouk alisisitiza bumuhimu wa kutekeleza majukumu Yao kwa umakini Katika kila eneo ikiwemo utunzaji wa vifaa vya uandikishaji hasa ukizingatia kuwa vifaa hivyo vimenunuliwa kwa gharama kubwa huku vikitaraji kutumika Katika Maeneo mengine .
0 Comments