Header Ads Widget

ANDENGENYE AWAPIGA MARUFUKU POLISI KUTUMIA NGUVU KUPITA KIASI KUKAMATA BODABODA

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye amepiga marufuku polisi kufanyia doria na shughuli za ukamataji za polisi kwa kutumia pikipiki zinazokamatwa na kuhifadhiwa vituoni kwa tuhuma za makosa mbalimbali ya kukiuka sheria za usalama barabara.

Andengenye ametoa kauli hiyo ya serikali katika kikao cha pamoja cha madereva bodaboda na viongozi wa kamati ya ulinzi za usalama za mkoa Kigoma na mamlaka za kusimamia sheria za usalama barabara kilichokuwa kikizungumzia changamoto iliyojitokeza baina ya polisi na bodaboda mkoani Kigoma.

Kutokana na malalamiko hayo yaliyotolewa na waendesha bodoboda hao Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa vielelezo hivyo vinapofikishwa kwenye vituo vya polisi ni marufuku kutumika kwa shughuli za polisi au askari binafsi na badala yake zibaki kama vielelezo hadi zitakapomaliza changamoto zilizojitokeza.

Sambamba na hilo Mkuu huyo wa mkoa amepiga marufuku polisi kutumia fimbo kukamata waendesha bodaboda, kurusha kwenye magari ya polisi pikipiki zinazokamatwa na hivyo kuharibika ambapo ametaka utu na staha kutumika wakati wa kuwakamata bodaboda hao.

Pamoja na hayo katika kikao hicho Mkuu huyo wa mkoa amewataka waendesha pikipiki hao kufuata sheria za usalama barabarani ikiwemo kuvaa kofia ngumu, kuwa na leseni, kulipia bima, pikipiki kuwa na vioo vya kuangalia nyuma (SIDE MIRROR), kuwa wasafi lakini pia kutokunywa pombe wanapokuwa kwenye shughuli hiyo ili hayo yakifanyiwa kazi hakutakuwa na changamoto kubwa baina ya bodaboda hao na polisi.

Baadhi ya waendesha pikipiki hao wakitoa malalamiko yao kwa Mkuu wa mkoa kwenye mkutano huo akiwemo Saidi Hussein wa eneo la Mgatutu alisema kuwa wanasikitishwa na polisi mkoani Kigoma  wanapokamatwa kwa kosa la kutokuwa na vioo vya kuangalia nyuma lakini wakienda polisi wanatakiwa kutoa shilingi 50,000 ambazo wanapewa maelekezo 10,000 kulipa kwa number ya malipo ya serikali na zinazobaki kuandika jina na kusaini kwenye daftari hivyo wana wasiwasi pesa hizo haziingii serikali bali polisi wanajinufaisha.




 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI