.Na Mwandishi Wetu, Shinyanga.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoani Shinyanga imetoa nakala ya wito wa kufika mahakamani kwa Afisa Madini Mkazi Mkoani hapa Daniel Mapunda ili kutoa ushahidi kuhusiana na shauri la madai namba 9/2023.
Madai hayo ni Kati ya Kikundi cha Tushikamane Gold Mine kilichopo Kitalu namba 4 katika Kijiji cha Nyaligungu Kata ya Mwakitoryo Wilaya ya Shinyanga, ambapo wadaiwa ni Kampuni ya Kichina yaTIAMTIN Investment Co LTD na wenzao wanaodaiwa kuwa ni waasi wa Tushikamane Gold Mine.
Kabla ya maagizo hayo Wakili msomi Paul Kaunda anayewakilisha wadai (Tushikamane Gold Mine) aliiomba mahakama kuwa wakati wa maandalizi ya wito huo ni vema ukaeleza bayana kuwa anayetakiwa mahakamani ni Afisa Madini Mkazi mwenyewe Mapunda na si kuwakilishwa na mtu mwingine.
Maoni hayo ya wakili yalikuja kutokana na Mapunda kuwakilishwa na mtumishi mwenzake mahakamani hapo siku ya Januari, 15, 2025, Jambo ambalo sio matakwa ya sheria.
Aidha katika shauli hilo wakili Kaunda aliiiomba mahakama ifute utetezi wote uliowahi kutolewa na upande wa wadaiwa (TIAMTIN Investment Co. ltd) kwa alichosema wameshindwa kuwasilisha majibu ya maswali kutoka kwa wadai kama inavyotakiwa kisheria.
Amesema majibu ya Maswali ya wadai yanapaswa kujibiwa na wadaiwa wenyewe na si wakili wao na akaongeza kuwa alichojibu wakili wa wadaiwa Shabani Mvungi tena bila kiapo ni kupotoka kisheria huku wakili Mvungi akidai Maswali hayo yamejibiwa.
Wlakili hapaswi kujibu Maswali ya wateja wangu, yanatakiwa yajibiwe na wadaiwa wenyewe lakini inaonyesha kuwa yamejibiwa na wakili tena bila kiapo kwa hiyo Maswali ya wadai hayajajibiwa" alisema wakili Kaunda na kuongeza;
"Mheshimiwa Hakimu niiombe mahakama yako ifute ushahidi wote ambao wadaiwa waliwahi kuutoa mahakamani hapa kwa sababu wamekinzana na matakwa ya sheria kwa kutojibu Maswali ya wadai" (Tupendane Gold Mine). alisema Kaunda.
Akijibu madai hayo wakili Mvungi aliieleza mahakama hiyo kuwa "Maswali ya wadai yamekwisha jibiwa kwa utaratibu unaostahili" akaiomba mahakama iyakubali majibu hayo.
Baada ya hoja hizo Hakimu Catherine Langau anayesikiliza madai hayo aliahirisha shauli hilo hadi Januari 20, 2025 atakapotoa maamuzi ya kesi hiyo.
Alipotakiwa Kufafanua zaidi nje ya Mahakama Wakili Mvungi hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo huku Wakili Kaunda mwakilishi wa Tupendane Gold Mine akasema " Tumeiomba Mahakama itoe wito kwa Afisa Madini Mkazi Daniel Mapunda ili atoe ushahidi wake" alisema na kuongeza;
"Tumeiomba Mahakama ifute utetezi wote wa upande wa wadaiwa kwa sababu hawajatekeleza takwa la kisheria la kujibu Maswali ya wadai kinyume na amri ya 11 ya Kanuni ya 7 ya sheria ya Mwenendo wa mashauli ya madai sura namba 33 ya 2019 inayosema"
'Kama Kuna kibali cha Mahakama cha kuleta majibu ya Maswali ya wadai wanatakiwa kuleta ndani ya siku 10 au muda wawaote ambao Mahakama itaona inafaa, lakini sasa Mahakama hakuna namna nyingine inatakiwa kufanya bali kufuta ushahidi wote uliwahi kutolewa na upande wa wadaiwa" alihitimisha Wakili Kaunda.
0 Comments