Header Ads Widget

WACOMORO WACHACHAMAA RAIS ASSOUMAN KUMRITHISHA MWANAWE MADARAKA

NA Mwandishi wetu,

MATUKIO DAIMA App, DAR ES SALAAM

KUNA vuguvugu la chini kwa chini katika visiwa vya Comoro baada ya Rais wa nchi hiyo, Azali Assouman kutangaza nia yake ya kumrithisha madaraka mwanawe.

Rais Assouman alitangaza hadharani nia hiyo hivi karibuni akiwa katika kisiwa cha Mohel kuwa atakapoondoka madarakani mwaka 2029 atamrithisha mwanawe, Nour El Fath.

Rais huyo alianza harakati za kumrithisha mwanawe mwaka mmoja uliopita baada ya kumteua kuwa msimamizi wa kuratibu masuala ya serikali, taarifa ambayo tayari imeibua sintofahamu juu ya hatima ya kisiasa ya nchi hiyo.

Baadhi ya wachambuzi na wanasiasa wameielezea hatua hiyo kuwa inaweza kuchochea vurugu na kutoweka kwa amani katika visiwa hivyo vilivyopo Bahari ya Hindi.

Baadhi ya wananchi wa Comoro waliozungumza na Matukio Daima wamesema hatua yar ais huyo kutangaza kumrithisha mwanawe ni ulevi wa madaraka na ukiukwaji mkubwa na katiba na inaweza kusababisha machafuko na uvunjifu wa amani nchini humo.

Mmoja wa wananchi hao, ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu za kiusalama, alikumbusha mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo yaliyofanywa na visiwa vinne ambapo kila kisiwa kinapaswa kutawala kwa miaka mitano tu.

Mwaka 2001 visiwa vitatu viliunda Katiba mpya ya Jamhuri ya Kiislam Comoro. Katiba hiyo pamoja na mambo mengine ilianzisha utaratibu wa mzunguko wa urais kwa miaka mitano yaani, The principal of rotating presidency between island for five years.

“Utaratibu huo ulianza vizuri ambapo (2002-2006) Rais Azali alitoka Grande, (2007-2011) rais alitoka kisiwa cha Anjouan ambaye ni Sambi na (2012 – 2016) Comoro iliongozwa na Dkt Ikililou Dhoinine kutoka kisiwa cha Mohel.

“Hatua ya Rais Assouman kutangaza kumwachia mwanawe madaraka imevunja katiba na hauonyeshi hatima iliyo njema kwa nchi yetu”alisema mwananchi huyo.  

Comoro inaundwa na visiwa vitatu vya Grande (Moroni), Anjouan na Moheli viliyopo Bahari ya Hindi. Hata hivyo kisiwa cha nne kilichokuwa miongoni mwa visiwa vya nchi hiyo wakazi wake walipiga kura mwaka 1974 na kuchagua kuwa sehemu ya koloni la Ufaransa.

Mwaka 2008 Jeshi la Wananchi wa Tanzania ilizima jaribio la kisiwa cha Anjouan kutaka kujitenga na kumwondoa kiongozi muasi, Kanali Mohamed Bakar na kisiwa hicho kurejea kwenye utawala wa Jamhuri ya Comoro.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI