Header Ads Widget

IRINGA WAPONGEZA TANESCO KUTATUA KERO YA TRANSFOMA POSTA


Mafundi wa Shirika la umeme Tanzania (TANESCO)Iringa wakibadili Transfoma ya eneo la Posta mjini Iringa linalohudumiwa wafanyabiashara wa Miyomboni na kuweka nguzo za zege leo picha na Matukio Daima media

NA MATUKIO DAIMA MEDIA 

WATEJA wa Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) eneo la kibiashara la Miyomboni mjini Iringa wamepongeza TANESCO kwa kusikia kilio chao na kutatua kero ya Transfoma lililokuwa likisumbua .

Wakizungumza na Matukio Daima media Leo  wateja hao walisema Transfoma hilo lililopo eneo la Posta mjini Iringa ni Moja ya Transfoma muhimu kwa wateja wa Shirika Hilo kupata Nishati ya umeme ila kero kubwa ilikuwa kulipuka mara Kwa mara kutokana na kuzidiwa Uwezo .


Hivyo walisema kupitia Chombo Cha Matukio Daima media na gazeti hilo  walilalamika na sasa Tanesco wameanza kutatua kero hiyo kwa kufunga Transfoma mpya

Matata Mduba ni mmoja wa watumiaji wa TRANSFOMA alisema kazi kubwa inafanywa na uongozi wa TANESCO mkoa wa Iringa kutatua kero hiyo na hivyo Wanapaswa kupongezwa kwa jitihada hizo.

"Transfoma hili ni muhimu sana kwetu wafanyabiashara na hili eneo ni la kibiashara hivyo kukosekana umeme ni kero kubwa sana kiuchumi lakini sasa tunauhakika wa kupata umeme wa Uhakika"

Pia tunapongeza ubunifu huu mkubwa wa kuja na nguzo za zege ambazo zitamaliza kabisa tatizo la nguzo kuharibika mara Kwa mara ama kuchomwa moto .


Mwenyekiti wa umoja wa Vijana wa Chama Cha mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Iringa mjini Isaack Kikoti alisema utatuzi wa Kero hiyo na nyingine ni Matunda ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ambayo pamoja na utekelezaji wake utatuzi ni sehemu ya utekelezaji.

Kwani alisema kazi nzuri inayofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kusogeza umeme mijini na Vijijini ni vema iende sambamba na ukarabati wa Miundo mbinu Pindi inaposumbua .

Hivyo alipongeza jitihada za uongozi wa TANESCO Iringa chini ya meneja wa TANESCO mkoa Mhandisi Grace Ntungi kwa kuendelea kufanya kazi kwa Kasi zaidi .

Kwa upande wake  Afisa Mahusiano wa Huduma kwa wateja TANESCO mkoa wa Iringa Donasian John Meja  alisema kuwa Moja kati ya wajibu wa TANESCO mkoa wa Iringa ni kuwasikiliza wateja na kuwajali .


Hivyo ubadilishaji wa Transfoma hiyo ni sehemu ya Majukumu ya Shirika katika kubadili Miundo mbinu chakavu na kuweka ya kisasa na kuwa Transfoma hiyo ilikuwa ikizidiwa na watumiaji hivyo inafungwa kubwa zaidi itakayotosheleza watumiaji wote .

Hata hivyo alisema zoezi la kubadili nguzo chakavu limekuwa likifanyika na kuwa nguzo hizo za zege wataendelea kuweka maeneo mbali mbali .

Aliomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa TANESCO na Kulinda Miundo mbinu ya umeme na kufichua wale wote wanaohujumu Miundo mbinu ya umeme .


TAZAMA FULL VIDEO BOFYA LINK HII

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI