Header Ads Widget

TANAPA YASHIRIKI MKUTANO WA “AFRICA ENERGY SUMMIT 2025 JIJINI DAR ES SALAAM

 


Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) linashiriki Mkutano wa Africa Energy Summit uliofunguliwa na Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Doto Biteko, ambaye pia ni Waziri wa Nishati nchini Tanzania jana tarehe 27.01. 2025 na kuendele hadi leo januari 28, 2025 katika Ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam. Ushiriki wa TANAPA ni katika kunadi vivutio vyake vyenye sifa tofauti za kuvutia kwa wageni hao.


Mkutano huo unaowakutanisha wakuu wa nchi zaidi ya 25 barani Afrika, ambapo mwenyeji wao ni Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umejikita kujadili na kuimarisha sekta ya nishati, hususan katika suala la kupanua upatikanaji wa umeme, kuboresha miundombinu ya nishati, na kutafuta suluhu za changamoto zinazokwamisha maendeleo ya sekta hiyo. 


Aidha, Mkutano huo pia unalenga kuvutia wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi katika sekta ya nishati, vyanzo mbadala kama vile jua, upepo, na gesi asilia. Hivyo, jukwaa hilo ni fursa kwa wadau mbalimbali, wakiwemo serikali, sekta binafsi, na mashirika ya kimataifa, kubadilishana uzoefu na mikakati ya kukuza matumizi ya nishati endelevu.


Ushiriki wa TANAPA katika mkutano huo una lengo la kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana katika Hifadhi za Taifa, pamoja na fursa za uwekezaji katika sekta ya utalii na uhifadhi nchini.


TANAPA inatumia jukwaa hilo kutoa mwaliko kwa jumuiya za kimataifa zinazoshiriki katika mkutano huo kutembelea Hifadhi za Taifa, ili kujionea vivutio vya utalii vinavyopatikana nchini Tanzania kama Mlima mrefu zaidi barani Afrika (Mlima Kilimanjaro), Kivutio cha Nyumbu wahamao katika Hifadhi ya Taifa Serengeti na Hifadhi nyingine zilizotawanyika kote nchini.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI