Header Ads Widget

PROF.MBARAWA AITAKA TPA KUBORESHA UTENDAJII BANDARI YA KIGOMA

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Waziri wa uchukuzi Profesa Makame Mbarawa ameitaka Mamlaka ya usimamizi wa bandari nchini (TPA) kuhakikisha inaweka na kusimamia mipango ambayo itaongeza upitishaji wa shehena kutoka nchi za maziwa makuu kwenda nchi za Ulaya  kupitia bandari ya Kigoma Kwenda bandari ya Dar es salaam.


Waziri Mbarawa alisema hayo alipofanya ziara kutembelea bandari ya Kigoma akiwa kwenye ziara ya kiserikali ya siku mbili  mkoani humo na kubainisha kuwa yapo mambo mbalimbali ambayo yasipowekwa vizuri yanaweza kuwakimbiza wafanyabiashara na kutumia bandari nyingine.

Alisema kuwa upo mzigo mkubwa wa madini, Magogo na mbao kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kupitia bandari ya Kigoma Kwenda bandari ya Dar es Salaam ili Kwenda nje ya nchi lakini kitendo cha mzigo kufika na kuchukua siku nyingi kwa kukosa mabehewa au sababu nyingine ni moja ya mambo ambayo yatakimbiza wafanyabiashara na wasafirishaji Shehena kutumia bandari za Tanzania na kutumia bandari za nchi nyingine huku akitaka pia suala la kodi liangaliwe upya.


Awali akitoa maelezo kwa Waziri Mbarawa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Juma Kijavara alisema kuwa mamlaka hiyo inaendelea na mkakati wa ujenzi wa gati ya kushusha na kupaki abiria katika bandari ya Kigoma ikiwa ni moja ya maboresho makubwa wanayofanya kwa kushirikiana na Serikali ya  Japan jambo litakaloongeza idadi ya abiria wa ndani na nje ya nchi.

Pamoja na hilo Kijavara akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TPA alisema kuwa wameshaingia mkataba na kampuni moja ya migodi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambao wamekubali kusafirisha madini yao Kwenda nje ya nchi kupitia bandari ya Kigoma na Dar es Salaam na kwa sasa wawekezaji hao  wamepewa eneo katika bandari ya Karema iliyopo mkoa Katavi ambapo wanajenga meli ya mizigo ambayo itakuwa ikisafirisha mizigo kutka DRC kupitia bandari ya Kigoma na Karema hivyo itawezesha kuongeza mzigo mkubwa kutoka DRC kupitia bandari hizo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI