Header Ads Widget

MSAADA WA KISHERIA BILA MALIPO KUANZA KUTOLEWA KIGOMA

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Waziri wa Katiba na Sheria na Katiba Dk.Damas Ndumbaro anatarajia kuzindua siku tisa za mpango wa usaidizi wa sheria bila malipo  kwa wananchi wa mkoa Kigoma ili kusaidia kukabili kutoa uelewa wa uendeshaji wa mashauri kwa wananchi wa mkoa huo.

Mkuu wa mkoa Kigoma,Thobias Andengenye akizungumza na waandishi wa Habari mjini Kigoma  alisema kuwa usaidizi huo wa kisheria unafanyika kupitia kampeni ya msaada wa kisheria wa Mama Samia ambao utaanza  Ijumaa Januari 24 hadi Februari 2  kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre mjini Kigoma

Andengenye alisema kuwa siku tisa za utekelezaji wa kampeni hiyo utaongeza uelewa wa namna wananchi wa mkoa Kigoma wanapaswa kusimamia mashauri yao mbalimbali kwa kufuata taratibu za sheria akieleza kuwa kesi za mirathi na ardhi zimekuwa zikichukua nafasi kubwa kwenye mashauri ya kesi mbalimbali mkoani humo.

Akitoa maelezo kwa Mkuu wa mkoa kuhusu kuanza kwa kampeni hiyo ya Msaada wa sheria wa Mama Samia Mkuu wa kitengo cha sheria wa wizara ya katiba na Sheria, Esther Msambazi  alisema kuwa awali yatatolewa mafunzo kwa maafisa maendeleo ya jamii, maafisa ustawi na wanasheria wa halmashauri za mkoa Kigoma ili kujua dhima na malengo ya  kampeni ya msaada wa kisheria wa Samia.


Msambazi akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wizara ya katiba na sheria, Eliakimu Maswi alisema kuwa hadi sasa kampeni hiyo  imefanyika kwenye mikoa 11 ikilenga kuwafanya watendaji hao wa halmashauri na wasaidizi wa kisheria kwenye mikoa mbalimbali kusaidia katika kukabili migogoro inayojitokeza kwa kutoa miongozi na ushauri watakaporudi kwenye maeneo yao kusaidia wananachi wa kipato cha chini wasio na uwezo wa kuajiri wanasheria ili kuwasaidia waweze kushughulia mashauri yao.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI