Header Ads Widget

MATOKEO KIDATO CHA NNE,ONGEZEKO LA UFAULU KISHYLE

 


NA ZUHURA ZUKHERY, MATUKIO DAIMA, IRINGA.   


    Wakati baraza la mitihani Tanzania likijivunia ongezeko la  ufaulu kishule  kwa asilimia 7.45 pia limewafutia matokeo wanafunzi 67 kwa udanganyifu wa mitihani ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa hatua za kimaadili kwa wanafunzi wa tano pamoja na wazazi kutokana na kuandika lugha za matusi katika karatasi za kujibia mitihani ya taifa ya kidato cha nne november 2024. 

Hayo yalisemwa leo  januari 23 2025 na katibu mkuu mtendaji wa baraza la mitihani Tanzania NECTA Dkt. Said Mohammed wakati akitangaza matokeo ya kidato cha nne ya wanafunzi waliohitimu kidato cha nne mwaka 2024 

Dkt Mohammed alisema kuwa suala hilo la wanafunzi kuandika lugha za matusi katika mithani yao huwa kunahatua  zinazochukuliwa moja kwa moja na baraza la mitihani kwa kuwafutia matokeo na kuziandikia barua shule walizosoma ili kuwasiliana na wazazi wao kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kimaadili.

Aidha dkt Mohammed alisema kuwa wamefuta matokeo ya wanafunzi wengine 62 kutokana na kufanya udanganyifu katika mitihani yao huku baraza hilo likikifungia kituo kimoja cha mtihani cha mkoani shinyanga kutokana na kufanya udanganyifu na kujaribu  kuhujumu mtihani wa kidato cha nne kwa mujibu wakifungu cha 48 chakanuni za mitihani cha mwaka 2024/2026 hadi baraza litakapojiridhisha kuwa kituo hicho ni salama kwa uendeshaji wa mitihani kitaifa.

Wakati huohuo  baraza la mitihani Tanzania NECTA limezuia matokeo ya wanafunzi 459 wa kidato cha nne mwaka 2024 kwa sababu mbalimbali zilizosababisha wasifanye mitihani huku baraza likiruhusu wanafunzi hao kufanya tena mitihani ya mwaka huu wa 2025..

Dkt Mohammed alisema kuwa wanafunzi hao wapo ambao hawakufanya mitihani yao yote pia wapo ambao hawakufanya idadi kubwa ya mitihani.

Akizungumzia ufaulu katibu mkuu huyo mtendaji alisema kuwa katika shule zote 5563 zenye matokeo shule 5552 sawa na asilimia 99.8 zimepata wastani wa daraja A hadi D ikiwa niongezeko la shule 218 ikilinganishwa na mwaka 2023, huku ongezeko la ufaululu kishule kukiwa na ongezeko la asilimia 7.45 kwa shule zilipata wastani daraja A-C  jumla 2494 sawa  na asilimia 44.83.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI