Header Ads Widget

PPRA WATAKIWA KUTOA ELIMU KWA TASISI NUNUZI NA WADAU WENGINE KUHUSU MFUMO WA NEST.


Zulfa alfani 

Matukio daima Mwanza 

Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA) wametakiwa kuendelea kuwajengea uwezo taasisi za nunuzi na wadau wengine kuhusu mfumo wa Nest ili kuboresha mfumo huo ikiwa ni katika kuweka mazingira rafiki kwa wazabuni kuweza kufikia malengo yalivyokusudiwa.

Hayo yamebainishwa Jijini Mwanza na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Mhandisi Chagu Ng'homa niaba ya  Mkuu wa Mkoa wa huo wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa serikali katika matumizi ya ya mfumo wa NeST.

Chagu amewataka wadau wa ununuzi nchini kutumia mfumo wa NeST ipasavyo ili kusaidia kupata wazabuni wenye gharama zinazolingana na thamani ya fedha zinazolipwa ili kuondoka changamoto ya kupata watu wasio na sifa.

"Mfumo huu umeletwa mahsusi ili kusaidia kuongeza wigo wa ushiriki wa wazabuni, kukidhi mahitaji na matarajio ya watumiaji pamoja na kurahisisha mchakato wabuombaji zabuni hivyo nendeni mkazingatie hayo ili kulisaidia Taifa." Chagu

idha ametowa wito Kwa Mamlaka hiyo kuhakikisha wanazichukulia hatuna za kisheria taasisi zote ambazo hazitumii mfumo wa NeST katika ununuzi kwani kutotumia mfumo guo ni kosa la jinai kama ilivyo katika Sheria ya ununuzi ya Mwaka 2023 kifungu Cha 128.

Meneja wa kujenga uwezo wa huduma za ushauri PPRA Gilbert Kamnde akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu ameleeza kuwa wameandaa mafunzo ya siku tano kutoka taasisi mbalimbali kuhusu elimu ya matumizi ya mfumo wa NeST  hasa katika monduri mpya zilizoanza kutumika.

"Kama mnavyofahamu PPRA Iko katika jukumu la kujenga mfumo mpya wa kielectonic wa manunuzi ya umma na tayari umeanza kufanya kazi tangu Mwaka 2023" Alisema Kamnde.

 Kwa upande wao baadhi ya washiriki walioshiriki katika mafunzo hayo wameeleza kuwa mfumo huo wa NeST utawasaidia katika utendaji kazi wao kutokana na changamoto wananzokumbana nazo wakati wa kufanya makubaliano ya tenda.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI