Header Ads Widget

POLISI YATAWANYA BODABODA KWA MABOMU YA MACHOZI KIGOMA

  

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

POLISI   mkoani Kigoma wamewatawanya kwa mabomu ya kutoa machozi waendesha pikipiki wanaofanya kazi ya kusafirisha abiria maarufu kama bodaboda kufuatia boda boda hao kufunga barabara mbalimbali za manispaa ya Kigoma Ujiji kupinga kile wanachodai ukamataji usio na kikomo unoafanywa na polisi.

Mmoja wa bodaboda hao Richard Benedictob aliyeongea kwenye eneo la tukio alisema kuwa 


 wamejikusanya na kuandamana kwenda ofisi ya Mkuu wa mkoa Kigoma Mnarani  kupinga manyanyaso ya polisi yanayowafanyakjushindwa kufanya kazi zao kwa uhuru.

Naye Ramadhani Lugodabi akizungumzia hali hiyo alisema kuwa wamechoka na hali hiyo kukamatwa kila siku na wanakaa vikao mara nyingi lakini usumbufu umekuwa mkubwa na wakienda polisi ni lazima watoe hela ndiyo pikipiki zao ziachiwe hivyo wameandamana kuonyesha hasira zao kwenye hilo na dunia ijue.

Hata hivyo kitendo hicho cha maandamano kimepingwa na Mwenyekiti wa Bodaboda mkoa Kigoma, Samwel Mtema ambaye alisema kuwa wameshafanya vikao vya pamoja baina ya polisi na bodaboda vikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa Kigoma, Abdulkadri Mushi kutafutia ufumbuzi changamoto zinazojitokeza hivyo maandamano hayo hayakuwa na haja yeyote ya kufanyika.

Akizungumza na waandishi wa habari eneo la ofisi ya Mkuu wa wilaya Kigoma mjini Kigoma, Kamanda wa polisi mkoa Kigoma,Filemon Makungu alisema kuwa polisi wanatekeleza majukumu yao katika kusimamia sheria na taratibu za usalama barabarani na wanakamatwa wote wenye makosa.

Alisema kuwa tayari walishakutana na kuzungumza na viongozi wa bodaboda hivyo haoni sababu ya kuwepo kwa maandamano hayo akibainisha kuwa licha ya kuzungumza nao kweny vijiwe mbalimbali bado boda boda wengi hawaja timiza suala la kuwa na leseni kwani wengi ni raia wa kigeni ambao vitambulisho vya taifa ambacho ni moja ya kigezo cha kupata leseni na kwamba operesheni hiyo ambayo ni ya kitaifa itaendelea.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI