Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Wakati maambukizi ya Virusi vya Ukimwi yakipanda mkoani Njombe na kufikia asilimia 12.7 kwa Mwaka 2024 toka asilimia 11.4 ya Awali Serikali imepongeza Jitihaza za Kuzifikia 95 tatu za Kupima,Kutumia dawa na Kufubaza virusi vya Ukimwi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe.Ummy Nderiananga ametoa kauli hiyo akiwa mkoani Njombe wakati kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi ilipozulu na kupokea taarifa ya hali ya Ukimwi ya mkoa.
Kwa mujibu wa Dokta David Ntahindwa kwa niaba ya Mganga mkuu wa Mkoa wa Njombe watu 66979 wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Ambao ni sawa na Asilimia 109 wamejitambua na wamechukua hatua mbalimbali za kuzuia maambukizi mapya.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe.Antony Mtaka amesema Mapambano dhidi ya Ukimwi yanapaswa kuendelea bila kupepesa macho kwani suala la unyanyapaa kwa sasa halina nafasi.
Elibariki Kingu ni Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Ukimwi yeye anasema Mkoa una Jukumu kubwa la kuyalinda makundi ya Vijana ili yasiingiliwe na hii itasaidia kupambana na maambukizi mapya ya VVU.
Wananchi mkoani Njombe akiwemo Happines Asukile wameiomba Serikali kuendelea kutoa elimu dhidi ya madhara ya unyanyapaa kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi kwani hakuna anayepanga kupata maradhi.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Ukimwi ipo Mkoani Njombe kwa ziara ya siku mbili ambapo Januari 10 mwaka huu inatarajia kutembelea kikundi cha watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi huko Mundindi wilayani Ludewa.
0 Comments