Header Ads Widget

MKUTANO WA NISHATI WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA, FURSA UTALII WA HISTORIA MAKUMBUSHO YA TAIFA



Makumbusho ya Taifa la Tanzania (NMT) imeshiriki kwenye mahojihano na kituo cha habari cha Star TV ikiongozwa na Mhifadhi historia Bw. Shomari Rajabu na Afisa Utalii Bi. Antonia Mnkama.

Kupitia kipindi hicho leo Januari 16,2025, imeweza kuongelea namna ambavyo NMT ilivyojiandaa kutumia fursa ya ugeni wa Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika kunadi vivutio pamoja na historia ya Taifa la Tanzania kwa wageni hao.

Kupitia mkutano huo utakaofanyika tarehe 27 na 28 Januari jijini Dar es Salaam, Makumbusho ya Taifa la Tanzania imejipanga kuwatembeza wageni wa mkutano huo katika maeneo ya kihistoria yanayopatikana jijini Dar es Salaam ikiwemo vituo vyake vya Kijiji cha Makumbusho na Nyumba ya utamaduni.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI