Header Ads Widget

MEZA YA MAGAZETI LEO ALHAMISI JAN 16/2025:RAIS SAMIA AFANYA TEUZI,BOMOA BOMOA IRINGA YACHAFUA HALI YA HEWA VILIO VYATAWALA BARABARA YAFUNGWA

 

MACHINGA IRINGA WAFUNGA BARABARA BAADA YA PICHA YA RAIS SAMIA KUCHANWA 

 NA MATUKIO DAIMA MEDIA,IRINGA

 WAFANYABIASHARA Ndogo Ndogo (Machinga) mjini Iringa na Vijana wanaojishughulisha na kazi ya bajaji wamefunga barabara ya MR -Mkwawa inayoelekea ofisi ya CCM mkoa wa Iringa wakipinga zoezi la Bomoa bomoa lililofanywa na Halshauri ya Manispaa ya Iringa usiku wa kuamkia Jana na kupelekea kuharibu picha ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan. 

 Wafanyabiashara hao walifikia uamuzi huo wa kufunga barabara Jana majira ya saa 5 asubuhi kama sehemu ya kushinikiza uongozi wa serikali ya wilaya na mkoa wa Iringa kufika kusikiliza kilio chao.

 Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi eneo la tukio wafanyabiashara hao walisema wanasikitishwa na uamuzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuvunja maeneo hayo na kama haitoshi kuharibu picha za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Hayati John Magufuli jambo ambalo si sawa . 

 Kwani walisema ilipaswa kuondoa picha hizo kwa heshima na kuzihifadhi kabla ya kuvunja maeneo hayo ama kuziondoa mara baada ya kuvunja maeneo yao. 

 Kwani walisema kitendo Cha kuharibu picha za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na kuvunja matawi ya CCM eneo hilo ni kukikosea heshima Chama Cha mapinduzi na serikali yake. 

 Alisema Yohana Sanga kuwa yupo kijana aliyehukumiwa jela ama kulipa faini milioni 5 kwa kuchoma picha ya Rais Dkt Samia ambayo aliichora mwenyewe sasa hawa Mgambo wa Manispaa ya Iringa wameharibu kusudi picha halisi za Rais Dkt Samia na Hayati John Magufuli. 

 Kwani alisema mbali ya picha hizo kufuatwa na Vijana wa UVCCM mkoa wa Iringa na kwenda kuzihifadhi ofisi za Chama ila kitendo kilichofanywa na mgambo hao si sawa na Wanapaswa kuwajibishwa kwa kutoheshimu picha za Rais ambazo ni tunu ya nchi na zinapaswa kuheshimiwa. 

 Hata hivyo Lukia Katema mkazi wa eneo hilo la MR mjini Iringa na Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Miyomboni alisema kuwa nyumba yake ni Moja ya maeneo yaliyoathirika kwa bomoa bomoa hiyo .

 Alisema kuwa usiku wa saa 10 Alfajiri ya kuamkia Jana alisikia Kishindo nje ya nyumba yake na baada ya kutoka  mgambo na maofisi ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wakiendesha zoezi la kuvunja Vibanda na nyumba yake.

 Alisema nyumba yake Moja kati ya chumba kimevunjwa na mgambo hao huku mali mbali mbali za wananchi waliovunjiwa zikiharibiwa wakati wa zoezi hilo. 

 Lukia alisema juzi ijumaa mgambo hao walifika eneo hilo na kuvunja maeneo hayo Kwa sehemu ila siku Moja kabla ya Jana kuvunjwa tena Mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada alifika eneo hilo na Kuwapa pole wahanga wa bomoa bomoa na kuahidi kulifanyia kazi Suala Hilo na kuwa hawatabomolewa tena . 

 "Meya alituhakikishia kuwa hatutabomolewa Vibanda vyetu tena ila usiku mgambo wamekuja na kubomoa "

 Alisema kuwa wafanyabiashara hao walipewe barua za kutakiwa kuvunja maeneo hayo Siku Moja kabla ya oparesheni hiyo na hawakuweza kufanya hivyo . 

 Hata hivyo wafanyabiashara wa eneo la Mashine tatu Jengo la maafuru la mama Sanga na eneo la RETCO mjini Iringa walihoji sababu ya Wao kuvunjiwa maeneo yao maana maeneo hayo wamekuwa wakiendesha kihalali na Manispaa ya Iringa iliwapatia leseni ya biashara . 

 Mwenyekiti wa umoja wa bajaji Iringa Melabu Kihwelo na Mwenyekiti wa Machinga Network Iringa Yahaya Mpelembwa waliomba uongozi wa serikali ya mkoa wa Iringa kuingilia kati zoezi Hilo kwani linaweza kuharibu taswira ya serikali iliyopo madarakani ambayo inahimiza wananchi wake kufanya kazi .

 Mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada alipotafutwa kwa njia ya simu pamoja na ofisini kwake alisema hawezi kulizulizungumzia Suala hilo kwani hajui chochote .

 "Mimi sielewi chochote juu ya oparesheni hii naomba aulizwe mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ama Afisa mipango miji "alisema Ngwada . 

 Hata hivyo jitihada za kumpata mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na ofisa mipango miji hazikufanikiwa baada ya kuwakosa ofisini . 

 Diwani wa kata ya Makorongoni Thadeus Tenga na diwani wa kata ya Miyomboni Kitanzini ambao ni wanazunguka maeneo yaliyovunjwa na mgambo hao walisema hakuna kikao chochote Cha Baraza la madiwani kilichoagiza oparesheni hiyo kufanyika .

 Huku diwani wa kata ya Ruaha Tandesi Sanga alisema kuwa wameitwa kwenye kikao Cha dharula na mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ili kujadili sakata hilo . 

 Huku akipinga vikali oparesheni hiyo kuwa haina Afya kwa wafanyabiashara hao na kutaka isitishwe na hatua Kali kuchukuliwa kwa wote waliohusika kuwasababishia hasara wafanyabiashara hao. 

 Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA)Jimbo la Iringa mjini Frank Nyalusi alisema kilichofanywa na mgambo wa Manispaa ya Iringa ni unyanyasaji wa wananchi na kuwa walipaswa Kuwapa muda wa kutoa mali zao badala ya kuziharibu .

 Nyalusi alisema Chadema Jimbo la Iringa mjini linasikitishwa na oparesheni hiyo pamoja na kuvunjwa kwa matawi ya CCM na kuharibu picha za Rais Dkt Samia kuwa si sawa .

 Alisema oparesheni hiyo kwa Vibanda vya wafanyabiashara imehusianaje na matawi ya CCM na kuharibu picha za Rais Dkt Samia na Hayati John Magufuli.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI