Na Hamida Ramadhan,Matukio Daima App Dodoma
WAZIRI wa Madini na Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde, amefanya uzinduzi wa Shina la wakereketwa la UVCCM katika Soko la Sabasaba, Jijini Dodoma.
uzinduzi huo unakwenda kuwasadia vijana hao wa bodaboda sehemu ya mapuumziko na kuondokana na adha ya jua na mvua adha ambayo waneipata kwa muda mrefu
Katika hotuba yake Waziri Mavunde ameahidi kuweka umeme na televisheni katika eneo hilo kabla ya Jumatano ijayo, hatua ambayo itawasaidia vijana kupata habari na kujifunza kwa urahisi na kusisitiza umuhimu wa vijana katika maendeleo ya Taifa na kuwapa motisha ili wajiandae kujiunga na shughuli za maendeleo.
Aidha, ameeleza kuwa atawaletea kisimbuzi cha Azam, ili vijana waweze kupata habari mbalimbali na kujifunza zaidi kuhusu masuala ya kijamii na kiuchumi.
Naye Katibu Mkuu wa UVCCM Jokate Mwegelo amemtaja Mavunde kama kiongozi bora anayewapa vijana motisha na mwangaza wa matumaini.
Jokate amesisitiza kwamba viongozi wanapaswa kuwa karibu na vijana na kuelewa changamoto wanazokabiliana nazo ili kuwasaidia katika kujenga mustakabali wao.
Katika kuunga mkono juhudi, Mwegelo alitoa shilingi milioni 3 kwa ajili ya kutunisha mfuko wa vijana wa Samia, akionyesha dhamira yake ya kusaidia shughuli za maendeleo na kuimarisha umoja miongoni mwa vijana.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na mamia ya vijana na viongozi wa UVCCM, ambao walijitokeza kwa wingi kuonyesha mshikamano wao na viongozi .
Sambamba na hilo Mavunde alihitimisha kwa kuwahimiza vijana kuchangamkia fursa na kushiriki katika mipango mbalimbali inayolenga maendeleo ya jamii.
0 Comments