Header Ads Widget

MAHAKAMA ZA TANZANIA KINARA UENDESHAJI MASHAURI AFRIKA

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Mahakama nchini Tanzania inaelezwa kupiga hatua kubwa katika kusimamia mashauri na kutoa haki kwa wakati  barani Afrika jambo linalozifanya nchi nyingi za Afrika kuomba kuja nchini kujifunza namna ya uendeshaji wa mashauri.


Waziri wa Katiba na Sheria,Dk.Damas Ndumbaro alisema hayo mkoani Kigoma  katika uzinduzi wa wiki ya sheria iliyofnyika kwenye viwana vya Mwanga Community Centre Mjini Kigoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya ufunguzi wa shughuli za mahakama nchini.

Waziri Ndumbari alisema kuwa akiwa kwenye kikao cha Mawaziri wa sheria kilichofanyika  Adis Ababa, Ethiopia kwenye makao makuu ya Jumuia ya viongozi hao wamepongeza utendaji kazi wa  mahakama ya Tanzania na mafanikio yake huku Morocco ikitajwa kufanya utafiti wa uendesha kesi katika nchi mbalimbali za Afrika na Tanzania kushika namba moja kwenye utafiti huo.


Akizindua wiki ya Sheria Mkuu wa mkoa Kigoma,Thobias Andengenye alisema kuwa maboresho ya mifumo, majengo na utendaji kazi wa mahakama ya Tanzania umeifanya mahakama kutekeleza majukumu yake kwa tija na kutimiza malengo ya dira ya taifa ya uboreshwaji wa shughuli za mahakama katika kusimamia utoaji haki huku akibainisha kuwa kuchelewa kutolea kwa hukumu za mahakama kuna athari kubwa katika kutekeleza mchakato wa maendeleo.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Kigoma Augustine Rwizile

Awali akizungumza katika uzinduzi huo Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Kigoma, Augustine Rwizile alisema kuwa katika dira ya 2025 hadi 2050 ya Tanzania tuitakayo uzinduzi huo unaibeba kwa vitendo ukibeba maono ya Raisi Samia katika kuhakikisha malengo ya dira yanafikiwa.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI