Header Ads Widget

JENGO LA KISASA LA BIASHARA LINATARAJIWA KUJENGWA WILAYA YA MULEBA.*

Na Mariam Kagenda _ Kagera

Shilingi Bilioni 1.7 zinatarajiwa kutumika katika awamu ya kwanza ya mradi wa ujenzi wa Jengo la Biashara linalojengwa eneo la soko kuu  wilayani Muleba mkoani Kagera ili kuwasaidia wananchi wa wilaya hiyo kujikwamua  kiuchumi .

Mkurugenzi mtendaji wa  Halmashauri ya wilaya ya Muleba Bwana Isaya Mbenje amesema hayo wakati wa hafla ya utiaji saini ujenzi wa Jengo hilo kati ya viongozi wa halmashauri na mkandarasi wa Intergo Company LTD kutoka jijini Dar_Es_Salaam.

Bwana Mbenje amesema kuwa mradi huo umepitia hatua kubwa  tatu ambapo hatua ya kwanza ilikuwa ni kusanifu hali ya udongo katika ardhi ambayo itajengwa jengo hilo,Kusanifu mradi na hatua ya tatu ni kupata mkandarasi ambaye ametoka Kampuni ya Intergo ambaye tayari amesaini mkataba wa ujenzi wa Jengo hilo kwa awamu ya kwanza ya jengo la mbele la ghorofa moja itakayokuwa na jumla ya Vyumba 84.

Ameongeza kuwa mradi huo utakuwa na awamu mbili ambapo awamu ya pili itakuwa ya majengo pacha ya nyuma na pembeni kuhakikisha mradi huo unakamilika na maandalizi yamekamilika ikiwa ni pamoja na taratibu za ununuzi.

Fedha za ujenzi wa mradi huo zinatokana na mapato ya ndani ya halmashauri hiyo na ujenzi unaanza leo na wanatarajia kukamilika kwa mradi huo Julai 25 mwaka 2025 .

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji   wa kampuni ya ujenzi ya Intergo kutoka Jijini Dar_Es _ Salaam  amesema kuwa Kampuni hiyo itahakikikisha inatekeleza kwa ukamilifu ujenzi wa mradi huo kwa muda waliokubaliana na Jengo hilo litakuwa mfano wa kuigwa katika mkoa wa Kagera .

Naye mgeni Rasmi katika Hafla hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Muleba Bwana Justus Magongo amesema kuwa azimio la kwanza katika halmashauri hiyo ilikuwa ni kupandisha mapato ya halmashauri  ambapo wakati wanaanza walikuwa wanakusanya shilingi Bilioni 4.8 na sasa wanakusanya Bilioni 8 hivyo kutokana na mapato hayo waliona wanaweza kutekeleza mradi mkubwa utakaoongeza thamani ya wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mradi huo.




 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI