Header Ads Widget

FILAMU ZA THE ROYAL TOUR, AMAZING TANZANIA ZIMEINGIZIA TANAPA MAPATO YA BILIONI 411 KWA MWAKA WA FEDHA2023/24

Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Nassoro Juma Kuji akichangia mdahalo wakati wa Hafla ya tukio la utangazaji wa takwimu za Idadi ya wataliii na mapato yatokanayo na utalii kwa mwaka 2024.

Kamishna Kuji amebainisha kwamba, wakati janga la COVID-19 lilipoikumba nchi yetu, Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) lilirekodi idadi ndogo sana ya wageni wa nje na kufanya mapato kushuka na kufikia kiasi cha billioni 57, lakini kupitia filamu ya Tanzania: The Royal Tour na Amazing Tanzania aliyoifanya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan TANAPA ikafikisha mapato billioni 411, kwa mwaka wa fedha 2023/24

Ambapo kwa sasa TANAPA imekusanya zaidi ya asilimia 80% ya mapato iliyopangiwa kukusanya kwa mwaka wa fedha 2024/25 ikiwa ni miezi 7 tu ya makusanyo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ndio Mgeni Rasmi katika Hafla ya tukio la utangazaji wa takwimu hizo za watalii na mapato kwa mwaka 2024.

T506USD#NiUtalliTena#CountMeIn#2025








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI