NI wazi kwenye siasa za Tanzania, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameibuka kama kiongozi mahiri, mwenye maono, na mtendaji anayeleta matumaini mapya kwa Taifa.
Uamuzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumpitisha Dkt. Samia kuwa mgombea urais na Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi ujao ni ushahidi wa heshima na imani kubwa waliyonayo wanachama na wananchi kwa kazi kubwa aliyoifanya.
Kuwa Rais Samia amedhihirisha kuwa siyo tu kiongozi wa maneno bali wa vitendo Katika kipindi kifupi cha uongozi wake, amefanikisha utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo inayogusa kila sekta.
Kutoka kwenye ujenzi wa miundombinu ya kisasa, kuboresha huduma za afya, elimu, na maji, hadi kushughulikia changamoto za kiuchumi, serikali ya awamu ya sita imeweka rekodi isiyo na kifani.
Miradi mikubwa kama Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP), reli ya kisasa ya SGR, na uboreshaji wa bandari ni mifano ya azma yake ya kuimarisha uchumi wa Taifa.
Pia, miradi ya kati na midogo imewafikia wananchi wa kawaida, ikiwa ni pamoja na maboresho ya barabara, vituo vya afya, na shule katika maeneo ya vijijini.
Kuwa hii inaonyesha kuwa hakuna mtu anayesahaulika chini ya uongozi wake.
Kuhusu Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi anasema ni kiongozi mwenye uzoefu na uwezo mkubwa.
Hivyo uteuzi wake kama mgombea mwenza ni ishara ya umoja na busara za uongozi wa CCM.
Anasema Sifa zake za utendaji, uadilifu, na kujituma katika nafasi mbalimbali za uongozi zinaimarisha timu ya Dkt. Samia. Kwa pamoja, wanaunda duo imara ambalo linaweza kuendelea kuleta maendeleo na ustawi wa Taifa.
Mlawa anasema upinzani nchini Tanzania umekuwa ukikabiliwa na changamoto za kujipanga na kuwa mbadala wa kweli wa CCM.
Sababu zifuatazo zinafanya wapinzani waendelee kubaki wasindikizaji kuwa ni Kukosekana kwa Ajenda Mbadala.
Anasema kuwa Upinzani umeshindwa kuonyesha mipango madhubuti ya maendeleo inayoshindana na mafanikio ya CCM.
Kwa mfano, serikali ya awamu ya sita imeonyesha wazi namna inavyoweza kushughulikia changamoto za kiuchumi kupitia uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu na huduma za kijamii.
Pili Wapinzani hawajawahi kuwasilisha mpango wa namna hiyo kwa vitendo kukosa Umoja na Mkakati imara.
Anasema kuwa tofauti za kiitikadi na ukosefu wa mshikamano miongoni mwa vyama vya upinzani ni kikwazo kikubwa.
CCM, kwa upande mwingine, imeonyesha mshikamano na nguvu za pamoja, kama ilivyoonekana katika uamuzi wa kumpitisha Dkt. Samia na Dkt. Nchimbi kwa kishindo.
Tatu Kazi Kubwa ya Serikali ya CCM katika Miradi ya maendeleo inayoonekana kila kona ya nchi inafanya wapinzani kukosa hoja za msingi za kushindana.
Aidha Kila Mtanzania anaona na kushuhudia miradi ya serikali ikibadilisha maisha yao, kutoka vijijini hadi mijini.
Sababu nyingine ni heshima kwa Demokrasia ya Ndani ya CCM kwani Uchaguzi wa ndani wa CCM ni mfano wa kuigwa.
Alisema kuwa utaratibu wa kuwapigia kura wagombea unawapa wajumbe nafasi ya kufanya maamuzi yenye busara na heshima.
Kuwa inawapa wananchi imani kuwa viongozi wa CCM wanachaguliwa kwa uwazi na kwa maslahi ya wote.
Akijibu swali kwa nini Wapinzani Wanapaswa Kumpa Hongera Dkt. Samia alisema Wapinzani wanapaswa kutambua mafanikio ya serikali ya Dkt. Samia na badala ya kupinga kila kitu, waunge mkono juhudi za kuwatumikia Watanzania.
Kuwa ni kwa sababu ya Umoja wa Kitaifa ambao Rais Samia amefanikiwa kuimarisha mshikamano wa kitaifa kwa kuzingatia maslahi ya kila Mtanzania bila kujali itikadi zao za kisiasa.
Pili kuhusu uwajibikaji na Uwiano wa Maendeleo kuwa Serikali ya awamu ya sita imeonyesha uwazi katika utendaji kazi wake na kuhakikisha kuwa maendeleo yanagusa kila eneo nchini.
Hivyo Wapinzani wanapaswa kuunga mkono juhudi hizi badala ya kuendelea na siasa za kupinga kila kitu.
Jambo jingine ni Fursa za Ushirikiano ambayo Serikali imekuwa wazi kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo, ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa.
Kuwa ni nafasi kwa wapinzani kuonyesha uzalendo na kushirikiana kwa manufaa ya Taifa.
Kwani alisema hakuna anayepinga kuwa kazi kubwa imefanyika hata wapinzani wanapaswa kukubali kuwa miradi ya maendeleo inayotekelezwa ni ya kihistoria na haina kifani.
"Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na mgombea mwenza Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ni viongozi wa matumaini na mabadiliko maamuzi ya CCM kumpitisha Dkt. Samia ni sahihi na yanawakilisha matakwa ya Watanzania walio wengi"
Mlawa anasema kwa kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya awamu ya sita, wapinzani hawana budi kubaki wasindikizaji.
Kuwa badala ya wapinzani kutumia muda Mwingi kupinga, wanapaswa kutenga muda Wao wa kumpa hongera Dkt. Samia, kuungana naye, na kushirikiana katika kuleta maendeleo ya kweli kwa Watanzania.
Kwani Taifa letu linahitaji mshikamano, si siasa za kugawanya watu na ni wakati wa kushirikiana kwa maslahi ya wote ,pia alisema Kwa upande wa Dkt Husein Mwinyi kwa Zanzibar mwenye macho haambiwe Tanzania Kila mmoja ni shahidi juu ya uchumi wa Bluu .
0 Comments