Leo Jumamosi Januari 25, 2025 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii. Dkt. Hassan Abbasi amekagua maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Nishati Afrika hasa maeneo ya kupendezesha ukumbi kwa taswira mbalimbali za wanyama na kazi inaendelea vyema.
Wakati huo huo,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabiti Kombo amesema kuwa viongozi wakuu wa Nchi wanaoshiriki mkutano wa nishati wa mission 300 wanaanza kuingia leo Januari 25,2025.
Ameongeza kuwa Tanzania imevunja rekodi kwa kuweza kuwa na mkutano unaowakutanisha wakuu wa Nchi takribani 25.
0 Comments