MKUU wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka leo januari 17 amewaongoza wananchi kwenye nguvu kazi ya ujenzi wa shule ya kwanza ya gorofa.
Shule hiyo inajengwa kwengwa kwenye Kata ya Kigera manispaa ya Musoma ikiwa na vyumba 8 vya madarasa.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo Chikoka amewashukuru wananchi waliojitokeza na kudai wameingia kwenye historia.
Amesema shule hiyo itakapo kamilika watakuwa wameingia kwenye historia kubwa ambayo haitaweza kufutika.
Chikoka amesema watahakikisha wanakamilisha msingi na kumuachia kazi mkandarasi aendelee na ujenzi.
" Leo ni siku ya historia kwa wananchi wote mliojitokeza kwenye zoezi hili na kwa wingi wenu mmeonyesha utayari wa kupokea shule hii.
" Ni Shule ya kwanza ya gorofa kwenye manispaa yetu ya Musoma na inaendelea kutupa heshima na kutoa nafasi kwa watoto wetu kusoma maeneo sahihi",amesema.
Mkuu huyo wa Wilaya amemshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuendelea kutoa fedha za miradi ya maendeleo ikiwemo ya elimu.
Kwa upande wao wananchi walioshiriki zoezi hilo wameshukuru kwa kupata mradi huo na watampa ushirikiano mkandarasi wakati wote wa ujenzi. In
0 Comments