Header Ads Widget

ASKARI WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA MAUAJI YA KIJANA NASHON KIYEYEU

 


NA MATUKIO DAIMA MEDIA 

ASKARI polisi mmoja na askari wa jeshi la akiba (Mgambo) Manispaa ya Iringa wamefikishwa Mahakamani na kusomewa shitaka Moja la mauaji ya kijana Nashon Kiyeyeu.

Washitakiwa hao askari polisi Kituo Cha Ipogolo mwenye namba XF4987 Sajenti Rojas Joshua Mmali na Thomas Mkembela askari mgambo walifikishwa Mahakama ya wilaya ya Iringa  leo majira ya saa 7 mchana huku Ulinzi ukiwa umeimarishwa katika viwanja vya Mahakama .

Akisoma maelezo ya kosa wakili wa serikali ofisi ya Taifa ya mashitaka mkoa wa Iringa Damas Sixtus  alisema kuwa washitakiwa hao walimuua Nashon Kiyeyeu Disemba 14 mwaka Jana katika eneo la Ipogolo .

Hata hivyo aliieleza Mahakama hiyo kuwa upelelezi wa Kesi hiyo bado haujakamilika.

Makimu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Iringa Adelina Faustino Ngwaya alisema washitakiwa hao hawatakiwi kujibu chochote watuhumiwa hao hawakupewa dhamana na Kesi hiyo imeahirishwa hadi February 4 mwaka huu itakapo tajwa tena.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI