Na Thobias Mwanakatwe,IKUNGI
MTU mmoja amefariki dunia na watu wengine 10 kujeruhi baada ya basi hilo kuligonga lori la mizigo kwa nyuma lilikokuwa limeegeshwa pembeni barabarani kutokana na kuharibika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Amoni Kakwale,akizungumza na waandishi wa habari leo amesema ajali hiyo imetokea Januari 25, 2025 saa 4:00 katika kijiji cha Nkuhi wilayani Ikungi mkoani Singida.
Amesema basi hilo lenye namba za usajili T 853 DHA ambalo lilikuwa limetokea Mbeya kwenda Mwanza liligonga kwa nyuma lori la mizingo lililokuwa limeegeshwa lenye namba RAH 587 D likiwa na tela lake lenye namba RL 10020 ambalo lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Kigari nchini Rwanda.
Kamanda Kakwale alimtaja kondakta wa basi aliyefariki kuwa ni Hamis Juma (27) mkazi wa Singida ambapo majeruhi wamelazwa saba wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida na watatu katika Hospitali ya Wilaya ya Ikungi.
Amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi kutochukua tahadhari na kuligonga lori hilo kwa nyuma ambaye alitoroka baada ya ajali kutokea na pia dereva wa lori naye ametoroka.
"Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka madereva wote wawili ambao walitoroka baada ya ajali na tunatoa saa 12 wajisalimishe katika kituo cha polisi na hata wasipojisalimisha watasakwa popote walipo, " amesema Kamanda Kakwale.
Kamanda Kakwale amewataka madereva wanapoendesha magari kuzingatia sheria za barabarani ili kuepusha ajali zisizokuwa za lazima.
Naye Muuguzi kiongozi wa zamu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida,Tabitha Mkumbo,amesema walipokea majeruhi saba wa ajali hiyo na kifo cha mtu mmoja ambaye miguu yote miwili ilikuwa imekatika.
Mkumbo aliwataja majeruhi hao ambao wanaendelea na matibabu katika hospitali hiyo kuwa ni Reoben Msigwa (32) mkazi wa Mwanza, Monga Kaluta (36) ambaye ni dereva wa basi mkazi wa Igona Mwanza ambaye alikuwa amelala na basi likiendeshwa na dereva mwenzake aliyemtaja kwa jina la Musa.
.Majeruhi wengine ni Hassan Shugape (31) mkazi wa Musoma,Aneth Samweli (18) mkazi wa Puma Singida, Razaki Ramadhani (28) mkazi wa Iyunga jijini Mbeya, Janeth Sambalu (35) mkazi wa Mafinga mkoani Iringa na Aisha Omary (22).
0 Comments