Na Matukio Daima Media, Dar es Salaam
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk. Suleiman Jafo amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amewekeza Dola za Kimarekani Billion 14 kwenye miundombinu ya Reli ya Treni ya Umeme (SGR) ili kiwarahisishia wafanyabiashara kusafirisha bidhaa zao katika soko la nje kwa urahisi.
Kauli hiyo aliitoa jana wakati akizundua bidhaa mpya ya African Fruti kwa ajili ya soko la kitaifa na kimataifa inayozalishwa na Kampuni ya Bakhesa Food Products Limited (BFPL).
"Hatuwezi kupata mafanikio nchini bila kufanya uwekezaji wa miundombinu, tuna kazi ya kuupandisha uchumi wa nchi yetu, Rais Samia tayari amewekeza Dola za Kimarekani Billion 14 katika reli ya SGR ili tupate soko la nje la uhakika kwa kufikisha bidhaa kwa wakati" alisema Dk. Jafo.
Alisema Serikali haina uwezo wa kujari vijana wote wanaohitimu fani mbalimbali lakini Kampuni ya Bakhesa Ina mchango mkubwa kwa kuwa imeajiri zaidi ya watu 10,000.
Akifafanua zaidi alisema wizara yake inategemea zaidi eneo la viwanda hasa binafsi kutoa ajira ya vijana, ubunifu wa bidhaa hiyo mpya unakwenda kuongeza mawasiliano ya moja kwa moja kutoka kwa mkulima mpaka mlaji.
Hata hivyo aliwataka wakulima nchini kkuchangamkia fursa ya kilimo cha zao la stafeli kwa kuwa bidhaa hiyo inahitajika zaidi sokoni kwa sasa.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa BFPL, Salim Aziz alisema kampuni hiyo tanzu kutoka Bakhesa Group, imefanya uwekezaji wa zaidi ya Sh. Bilioni 700 kwa mwaka 2023/2024 na kwamba imechangia na kulipa kodi Sh. Bilioni 180 katika kipindi hicho.
"Kampuni hii inasindika matunda zaidi ya tani 45,000 kwa mwaka yenye thamani ya zaidi ya Sh. Bilioni 25 kutoka soko la wakulima wa matunda wa ndani zaidi ya 150,000 yakiwamo Maembe, mananasi, machungwa,ukwajua,na pasheni"alisema Aziz.
0 Comments