Header Ads Widget

SILAA: BODI TTCL SIMAMIENI SHIRIKA LIENDESHWE KIBIASHARA



Na Matukio Daima Media, Dar es Salaam 


WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa ameitaka Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kusimamia vizuri shirika hilo na ikiwamo kuhakikisha linaedeshwa kibiashara pamoja na kuleta tija kwa uchumi wa nchi.


Pia amemuagiza Mwenyekiti wa Bodi hiyo, David Nchimbi kutengeneza mpango utakaolitoa Shirika lilipo sasa na kulipeleka kwenye uendeshwaji kibiashara ikiwa ni sehemu ya kutekeleza maagizo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.


Silaa alitoa kauli hiyo leo Desemba 16,2024 jijini Dar es Salaam wakati akizindua Bodi ya TTCL na kuitaka kutambua kuwa shirika hilo ni kubwa lililotangulia kwenye sekta ya mawasiliano nchini na kwamba serikali imewekeza fedha nyingikwa matumaini ya kulikuza zaidi.



"Baada ya Rais Samia kuapisha mawaziri Zanzibar alielekeza kwamba mwenye dhamana ya kusimamia shirika na kuhakikisha linaendeshwa kibiashara hivyo Mwenyekiti wa Bodi utengeneze mpango utakaotutoa tulipo na kutupeleka kuliendesha kibiashara na kutekekeleza maelekezo ya Rais " alisema.


Alisema Serikali imewekeza fedha nyingi kwenye miundombinu ya mawasiliano ya Taifa ikiwamo mkongo wa taifa ambao umeunganishwa nchi nzima, miradi mbalimbali mikubwa ya mawasiliano ikiwamo wa kituo cha Taifa cha data hivyo ni nia ya Rais Samia kuona uwekezaji huo mkubwa uliofanywa kwa fedha za wananchi uweze kuleta tija kwa kujiendesha kibiashara na kuiona ile thamani ya fedha iliyotolewa.


Aidha alisema kwamba Shirika likiendeshwa vyema linaweza kukuza sekta mbalimbali na kuleta mapinduzi makubwa kwenye uchumi wa nchi.


"Nawasihi, Mwenyekiti na wajumbe tekelezani hayo na ninawaahidi milango ya wizara iko wazi, na mtambue uendeshaji wa shirika uko chini ya bodi hivyo uwajibikaji uko chini ya mabega yenu siimamieni menejimenti vizuri ili tufike tuendako" alisema Waziri Silaa.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi hiyo, Nchimbi anamhukuru Rais Samia  

 kumteua katika nafasi hiyo na kuahidi kuwa ataiongoza Bodi vyema ili kuwa na shirika jipya na kulipeleka mbele zaidi na kwa kasi.


"Tunatambua kiu ya Watanzania ni kuliona shirika lao likifanyakazi kwa weledi na kusonga mbele zaidi" alisema Nchimbi.


Alisema wajumbe wana uwezo mkubwa na wamesikia maelekezo yaliyotolewa na watayafanyia kazi hakuna litakalowashinda 







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI