Na,Jusline Marco:Tanga
Serikali imetoa Tani 22.5 za mahindi kwa kaya 125 za wananchi zilizokubali kuhama kwa hiari kutoka ndani ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Kijiji cha Msomera Handeni Tanga.
Wananchi hao wameendelea kunufaika kwa upatikanaji wa mahindi yanayotolewa na Serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Lengo la ugawaji wa mahindi hayo ni kuwasaidia wananchi waliohamia kijijini hapo hivi karibuni kupata chakula kwa miezi 18 ijayo wakati wakiendelea kuandaa mashamba kwa ajili ya kilimo.
Mahindi hayo yametolewa gunia mbili kwa kila kaya katika kaya 125 ambapo Kaya hizo zinajumuisha kaya 23 zilihamia Msomera tarehe 19 Desemba, 2024.
0 Comments