Naibu waziri wa Wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum Mhe. Mwanaid Ally Hamis amefungua mafunzo ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2024 katika Halmashauri ya wilaya ya Mbeya na kuwakutanisha viongozi mbalimbali wa vijiji, vitongoji na kata wilayani humo.
Akizungumza na viongozi mbalimbali wilayani Mbeya Naibu Waziri huyo amesema ni muhimu matokeo ya sensa kujulikana kwa wananchi na Serikali ili kujua namna ya kuratibu shughuli za maendeleo ambapo ameitaka ofisi ya Taifa ya takwimu (NBS) kuendelea kutoa elimu hiyo kwa jamii kwa maendeleo endelevu.
Amesema ufunguzi wa mafunzo ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 ni kwa ajili ya maendeleo ya wananchi bila kujali itikadi zao za kisiasa wala kidini bali ni suala la kitaifa.
"Matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 ni kwa ajili ya maendeleo yetu, dira hii ni yetu sote so kila mwananchi anapaswa kushiriki kutoa maoni kwa ambao tumeshapata elimu hii pia tuitikie wito huu viongozi wote tukiongozwa na Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya maendeleo yetu", amesema naibu waziri Mwanaid.
Kwa upande wake Mbunge wa Mbeya vijijini Mhe. Oran Manasse Njeza amesema matokeo hayo ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ambapo ametumia fursa hiyo kumuomba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwasaidia wanafunzi mashuleni kuwa na maabara kwa ajili ya masomo ya teknolojia ya habari (TEHAMA) pamoja na uboreshaji na ujenzi wa barabara kadhaa katika jimbo lake ili kuwasaidia wananchi ambao kwa asilimia kubwa ni wakulima na wafanyabiashara..
0 Comments