Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Vijana mkoani Njombe wameonywa juu ya kujiingiza kwenye biashara haramu zikiwemo za kuuza miili yao,Kutumika kusafirisha dawa za kulevya na kujihusisha na matukio ya kijambazi na badala yake wachangamkie fursa zilizopo katika maeneo yao kupitia utaalamu wanaosoma vyuoni.
Onyo hilo limetolewa na Mhandisi Eliud Nyauhenga Mdau wa elimu mkoa wa Njombe akiwa mgeni wa Heshima katika Mahafali ya 13 ya chuo cha Aman Chini ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kusini Njombe ambapo amewataka wahitimu kwenda kuzigeuza changamoto kuwa fursa huko uraiani na kujiepusha na biashara haramu.
Mhandisi Nyauhenga amesema Vijana wengi wa Kitanzania wamekuwa wakitumika vibaya kwa kusafirisha dawa za kulevya,kugeuza miili yao kuwa biashara ukiwemo ushoga kwa kisingizio cha ugumu wa maisha jambo ambalo linapaswa kupigwa vita kwa kutumia elimu waliyoipata katika kuziendea fursa na biashara halali.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la kilutheli Tanzania KKKT Dayosisi ya kusini Njombe Dokta George Fihavango Amewataka vijana kujiandaa na mabadiliko ya Teknolojia yanayouandama ulimwengu wa sasa kwani Hakuna namna ya kukabiliana nayo zaidi ya kusoma na kujifunza.
Katika Mahafali ya 13 hayo Askofu Fihavango amesema Kwa kufanya hivyo itakuwa rahisi kuendesha maisha Kutokana na fursa nyingi zilizopo na hivyo kinachotakiwa ni kukubali kubadilika kifikra na kuyapokea mabadiliko ya Teknolojia.
Mwalimu Fredy Ngimbudzi ni mkuu wa chuo cha hicho,katika taarifa ya chuo amesema wanatarajia kuongeza udahili wa wanachuo toka 136 waliopo sasa hadi 250 ili kupanua wigo wa elimu na kukuza ustawi wa katika jamii.
Hata hivyo wahitimu wa chuo hicho wanasema watakwenda kutumia elimu walioipata kukabiliana na changamoto za ajira ili kuepukana na Magenge yanayoweza kuwaingiza matatizoni.
0 Comments