Na Hadija Omary
Lindi
Mtandao wa jinsia na Maendeleo Tanzania (TGNP) umewakutanisha Watendaji wa Kata na maafisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya Manispaa ya Lindi Mkoni humo kuwajengea uwezo wa namna ya kuingiza Bajeti yenyemtazamo wa kijinsia kwenye mipango na Bajeti Ngazi za mitaa, vijiji na Kata .
Akizungumza Katika kikao kazi hicho mwezeshaji wa maswala ya jinsia na Maendeleo kutoka mtandao wa jinsia na Maendeleo TGNP Scola Makwaiya Amesema TGNP Inatekeleza Mradi wa uwezeshaji wanawake kushiriki uongozi na ushiriki wa haki za kiuchumi kwa kushirikiana na Shirika la umoja wa mataifa kitengo cha wanawake .
Amesema Mradi huo unatekelezwa Katika mikoa minne ambayo ni Mtwara, Lindi, Dar es salaam na Pwani huku Akieleza miongoni mwa sababu zilizowasukuma kutekeleza Mradi huo ni pamoja na uwepo wa Bajeti zinazotengenezwa kutozingatia mahitaji maalumu .
Hata hivyo Bi Makwaiya ameeleza malengo mahusisi ya kikao kazi hicho kuwa ni Kujenga uelewa wa pamoja kuhusu dhana za jinsia zinazohusu Bajeti yenye mlengo wa wa kijinsia, kuimarisha uwezo wa mamlaka za Serikali za mitaa Katika uchambuzi wa kijinsia na Umuhimu wake.
Kufanya uchambuzi shirikishi wa Bajeti ya Wilaya 2024/2025 ili kubaini maswala ya kijinsia yaliyoingia kwenye Bajeti , mapungufu na kuondoa mpango kazi na kuingiza maswala ya jinsia kwenye Bajeti ya 2025/2026 ya Manispaa pamoja na kuandaa na kujenga nguvu ya pamoja.
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi hicho wameeleza kuwa TGNP imewasaidia kuwaongezea uelewa na Umuhimu wa kutenga Bajeti zenye mlengo wa kijinsia Katika Maeneo yao.
" Kiukweli wametuongezea kitu maana hapo mwanzo tulikuwa tunatengeneza tu bila kuzingatia huu usawa wa kijinsia lakini baada ya kupata Mafunzo haya yatazidi Kuboresha pale tunapotengeneza Bajeti zetu kuzingatia ule usawa wa kijinsia kwenye kila eneo" alisema Ally Mohammed Kaimu mtendaji Kata ya mchinga.
0 Comments